Maofisa ofisi ya wakala wa vipimo watinga maonyesho ya madini geita

Mkurugenzi wa huduma za Biashara wa Wakala wa vipimo Deogratius  Maneno akizungumza mbele ya waandishi wa habari pichani Kwenye maonyesho ya tano ya kitaifa ya Madini yanayofanyika mkoani Geita
Mkurugenzi wa huduma za Biashara wa Wakala wa vipimo Deogratius  Maneno akizungumza mbele ya waandishi wa habari hawapo pichani. Kwenye maonyesho ya tano ya kitaifa ya Madini yanayofanyika mkoani Geita

 Na David John 

MKURUGENZI wa Huduma za Biashara wa wakala wa vipimo Deogratias Maneno Amesema taasisi hiyo ipo chini wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Jukumu kuu walilonalo ni kumlinda mlaji kupitia matumizi sahihi ya  vipimo.

Amesema kuwa jukumu lingine ambalo wanalo katika mkoa wa Geita Serikali ilijenga Masoko ya Dhahabu na kazi yao kwenye vituo hicho nikwenda kuhakikisha ubora wa vipimo kwa maana ya midhani.

Deogratius Ameyasema hayo leo Oktoba 6 mwaka huu kwenye Maonyesho ya Tano ya kitaifa ya Teknolojia  ya Madini yanayofanyika mkoani humo .ambapo amesema katika mkoa wa geita kuna vituo nane na kwenye hivyo vituo kuna midhani inayotumika kupimia madini ya dhahabu hivyo wanakwenda hapo kuhakiki vipimo sahihi vya midhani.

“Tunashukuru kwa watu wa sekta ya madini wamepata uelewa na sasa wanatumia midhani ambayo ni midhani maalumu kwa ajili ya kupimia na serikali imetuwezesha sisi wakala wa vipimo kupata vifaa maalumu vya kuweza kuhakiki midhani hiyo na vifaa vinavyotumika ni maalumu kuliko vile vya kawaida na ni vya hali ya juu na gharama yake ni kubwa.”amesema 

Nakuongeza kuwa “Vilevile tumepita kwa wachimbaji wadogo wadogo na kuweza kuwapa elimu juu ya vipimo,na tumejaribu kuwapa elimu kwamba kila wanapopima wasijalibu kuiamini hiyo midhani hivyo basi jaribu kutumia mdhani wa mwingine ili kuona ulinganifu na ukigundua una tatizo wasiliana na wakala wa vipimo.”amesisitiza

Deogratius Ameongeza kuwa kazi ya wakala wa vipimo ni kutoa maelekezo kwamba ni mdhani gani utumiwe au nini kifanyike hivyo kwenye eneo hilo wanafanya hivyo lakini kwaupande mwingine wakala wa vipimo wanamaeneo mapya ambayo wanashukuru serikali wameyaza kuyatekeleza na wameaza kumlinda mlaji.

Amefafanu kuwa pia wakala wa vipimo wanakagua mita za maji kwa sababu sehemu kubwa za mita za maji za majumbani zimekuwa za zamani na katika mahusiano yao na Serikali wamekubaliana na wezao wanaaza kujikita kwenye mita mpya na wasiende sana kwenye mita za zamani na pale ambapo  kwenye baadhi mikoa imeshaweka utaratibu nzuri wa mashiriukiano kati ya mamlaka ya maji na wakala wa vipimo kwa lengo la kukagua m ita hizo.

Pia amesema kuwa wameaza ukaguzi kwenye upande wa mita za umeme zinazozalishwa kwenye viwanda vya ndani ya nchi na baadhi ya mita zimeshakagulia hadi sasahivi na baadhi mitambo ya mita iko Kibaha Misugusugu kwa ajili ya kuhakiki na mwingine upo mkoani kilimanjaro na ule wa kilimanjaro kazi yake kubwa ni kama sehemu ya rufaa na wa misugugusu ni wamatumizi ya kila siku.

Ameongeza kuwa midhani mingine ni ya kawaida ambayo wanafanya kwenye bidhaa za kufungasha na lengo la msingi nikuona kuwa mtu ananunua na anapata thamani ya fedha yake na wamepata nafasi ya kuona wajasiriamali wengi na wameshaongea nao na wamepata maelekezo kutoka kwa viongozi wao na kwakipindi kifupi kijacho watafanya nao mafunzo maalumu na kuwapa elimu ya ufungashaji bora na kuhusu maonyesho hayo amesema ni muhimu sana kwani watu wanapata kujifunza mambo mbalimbali.

Deogratius Ameongeza kuwa watakuwa na kipindi maalumu kwa watu wa geita ili kuwaelimisha hasa wajasiliamali wadogo wadogo kwenye eneo la ufungashaji wa bidhaa kwa lengo la kuongeza uwezo wao na bidhaa zao kutambulika kimataifa.