Watu wawili wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Geita kwa tuhuma ya kumuua kwa kumchinja Mwanamke Mmoja alietambulika kwa jina la Butamo Igonzele (70) Mkazi wa kijiji cha Bumegezi Kata ya Ihanamilo wilaya ya Geita Mkoani Geita.
Akizungumza na Wandishi wa Habari Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Polisi Berthaneema Mlayi amesema watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo kwa ajili ya upelelezi wa kina ili kubaini wahusika.
Amesema watuhumiwa hao wamemakatwa baada ya uchunguzi wa awali kuonyesha wanaweza kuhusika katika mauaji hayo huku jitihada zikifanyika katika kujiridhisha kupitia uchunguzi wa awali.
Kaimu Kamanda amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Joyce Julius ambaye ni Mtoto wake na Marehemu na Juma Charles ambaye ni Mkwe wa Marehemu ambao inadaiwa walikuwa wanamtuhumu Marehemu kuhusika na kifo cha mtoto wao ambaye alifariki wiki Moja iliyopita