Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Netho Ndilito Kwa niaba ya timu ya uongozi wa Halmashauri (CMT) amemkabidhi gari ya kisasa aina ya LANDCRUISER Mpya yenye thamani ya Milioni 170 mwenyekiti wa halmashauri hiyo Festo Mgina ili liweze kusaidia kutoa huduma kwenye vituo vya afya na hospitali zilizoko katika halimashauri hiyo
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mufindi Festo Mgina ampongeza mkurugenzi wa halmashauri ya Mufindi Netho Ndilito pamoja na watendaji wake kwa kuweza kufanikisha ununuzi wa gari la kisasa la kubebea wagonjwa kwa wakati ambalo litasaidia kupunguza changamoto ya vifo hasa vya kina mama na mtoto kwenye halimashauri hiyo.