Mwili wa robert mugabe kuwasili zimbabwe leo

Mwili
wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyefariki dunia Ijumaa
unasafirishwa leo kurejeshwa nyumbani kutoka Singapore kwa ajili ya
mazishi.

Mugabe ambaye alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95 , alikuwa hospitalini kwa matibabu nchini Singapore.

Taratibu za kitaifa za kuuaga mwili wake zitafanyika siku ya Jumamosi , kabla ya kuzikwa kijijini kwao Jumapili.

Robert
Mugabe, ambaye alikuwa kiongozi wa vita vya msituni ambaye aliiongoza
Zimbabwe baada ya Uhuru mwaka 1980, aling’olewa madarakani  mwaka 2017

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *