RAIS
Dkt. John Pombe Magufuli amewashukuru viongozi na waumini wa dini ya kiislamu pamoja
na wa dini nyingine nchini kwa kuliombea Taifa katika kipindi cha miaka mitano
ya awamu ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano na amewasihi waendelee na
utaratibu huo.
Kauli
hiyo imetolewa leo (Ijumaa, Novemba 27, 2020) baada ya kuswali swala ya Ijumaa
katika msikiti wa Msalato jijini Dodoma. “Wakati najiandaa kuja kuswali
nilimuaga Mheshimiwa Rais na ameniagiza nilete salamu zenu kwamba anawashukuru
sana kwa kumuunga mkono.”
Waziri
Mkuu amesema: “Rais Dkt. Magufuli amesema mbali na viongozi hao na waumini kumuunga
mkono katika awamu ya kwanza ya uongozi wake, pia walitoa ushirikiano mkubwa
katika kipindi cha kampeni kwa kuendelea kuliombea Taifa hadi uchaguzi ukafanyika
kwa amani.”
Waziri
Mkuu amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli amewaomba viongozi hao wa dini
pamoja na waumini waendelee kuliombea Taifa na viongozi wake ili waweze
kutekeleza majukumu yao kwa amani na utulivu.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi hao
waendelee kuwahamasisha waumini washiriki ibada mbalimbali kwa sababu jambo
hilo ni muhimu na linapaswa kufanyika kwa kuzingatia muda. “Kuswali ni muhimu,
wahamasisheni waumini kushiriki katika ibada.”
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwasihi waumini hao wawazoeshe watoto wao kufanya ibada ili wawe
watoto wema. Pia aliwasihi viongozi wa msikiti huo waimarishe kitengo cha elimu
na watumie nyumba za ibada kupata mawaidha mbalimbali.
Awali, Imamu wa msikiti wa Msalato, Sheikh
Aboubakar Abdallah Omar alitumia fursa hiyo kuwasisitiza waumuni juu ya umuhimu
kuishi kwa unyenyekevu na kumtegemea Mwenyezi Mungu katika maisha yao na
wajiepushe na vitendo vya ufisadi.
(mwisho)