Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) , Rais John Magufuli amewataka viongozi wa
mikoa wa chama hicho kutokuwa na majina yao mfukoni katika mchakato wa
kura maoni kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge.
Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020 jijini Dar es
Salaam alipokutana na viongozi wa mikoa, wilaya na jumuiya za chama
hicho kutoka mikoa yote nchini.
“Nawashukuru
sana wajumbe, kwa kweli leo nina raha sana, na kama ndugu Bashiru
unafikiri lolote baya leo hakuna baya shetani ameshindwa. Leo ni siku ya
raha ya kukutana na Chama kikubwa kilichoshika hatamu ya uongozi wa
Taifa hili.
“Niliona tukutane hapa kwanza tukishamaliza hapa tutakwenda Ikulu kupiga
picha na kama kuna maji tutakunywa wote pamoja, Ikulu ni yenu na ninyi
ndiyo mlinipeleka Ikulu ahsanteni sana.
“Eneo la fedha na uchumi tumeweza kuchukua hatua mbalimbali kuhakiki,
kurejesha na kuthaminisha upya mali na rasilimali za Chama, na jitihada
hizo zimeongeza mapato kutoka Tsh Bil 46.1 hadi mwaka 2015/16 hadi tsh
Bil 59.8 mwaka 2018/19.
“Baada ya tathimini na shughuli ya uhakiki wa mali za Chama, thamani
yake imepanda kutoka Bilioni 41.033 Mwaka 2016/2017 na kufikia Bilioni
974.66 mwaka 2020, ongezeko la asilimia 2275.3%. Tathmini hii ni ya
mikoa13 tu na kazi bado inaendelea.
“Niwaombe
Viongozi wenzangu ndani ya Wilaya na Mikoa wakati wa mchakato wa
uchaguzi tusiende na majina mfukoni tuoneshe ukomavu mwaka huu, tuwaache
wengine wakurupuke kuvunja taratibu wagombane, tusikate majina ya
Wagombea kwasababu zetu binafsi
“Mtu unajijua ni Mchezaji mzuri unaficha chenga zako kwanini?, tujiandae
na uchaguzi, CCM hii sio ile ya nyuma na Wapinzani wetu sio wale wa
nyuma, Wapinzani wamebadilisha mikakati yao, mingine wanaiweka hadharani
na mingine ni ya kificho, tusibweteke
“Fedha zilizopo sasa hivi tuna uwezo wa kuendesha nchi kwa miezi 6,
hatakama tusipokusanya leo hela tunaweza kuendesha nchi kwa miezi 6
ndiyo maana tunapata fedha za kujenga miradi mikubwa.
“Wala pasitokee Kiongozi yoyote ndani ya Serikali atakaye sema Chama
kinanifatafata, lazima Chama kikufate kama hutaki kufatwa ondoka upishe
tuweke watu wengine.
“Hatutaki Chama hiki kuwa ombaomba ambacho kinategemea matajiri ambao
baadae wamekuwa wakikiweka Chama mfukoni. Serikali iliyopo madarakani
leo ni ya CCM. Viongozi niliyowateuwa wote, ujue unakwenda kutekeleza
masuala ya ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
“Watendaji wa serikali nataka kutoa wito na Waziri Mkuu uko hapa,
wasisitizeni viongozi wa serikali walioko madarakani chama lazima
kitawafuata, chama lazima kiangalie matokeo halisi ya miradi
inayotekelezwa kule.
“Tuliomba mikopo hawakutupa, tukabana fedha za mafisadi tukajenga
wenyewe, huu mradi wa umeme ndugu zangu umepigwa vita sana lakini
ulikuwa unapigwa vita kwa sababu watu walikuwa wana interest ya Selou.
“Idadi ya Watalii wameongezeka kutoka Mil. 1.1 mwaka jana hadi zaidi ya
Mil. 1.5, tunataka tujenge uchumi wa nchi iliyo tofauti, lakini hata
kuzaana hatuko nyuma, kuzaa ni uchumi msidanganywe.
“Mwezi Februari Tanzania itaanza Safari za Ndege kutoka Nchini kwenda
China moja kwa moja. Ndege nyingine zinakuja na tumenunua kwa fedha
taslimu. Tajiri huwezi kununua kwa kukopa,” amesema Rais Magufuli.
==>>Msikilize hapo chini