Rais wa malawi amvua madaraka naibu wake kwa wizi wa mamilioni ya pesa

 

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera(kulia) alimvua madaraka makamu wake Saulos Chilima(kushoto) kwa kutajwa katika ufisadi. Picha: Getty Images. 

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera Jumanne, Juni 21, alimvua madaraka makamu wake Saulos Chilima baada ya kuhusishwa na kashfa ya ufisadi ambayo imeitikisa nchi hiyo. 

Chakwera alisema uchunguzi wa ulaghai wa manunuzi wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa nchini humo (ACB) uligundua kuwa maafisa 53 wa umma wa sasa na wa zamani walipokea pesa kutoka kwa mfanyabiashara Mwingereza ambaye pia ni raia wa Malawi Zuneth Sattar kati ya Machi na Oktoba 2021.