Raisi samia kufungua mkutano wa utalii arusha leo

Waziri wa utalii Pindi Chana akisisitiza jambo mapema jana

 Raisi Samia kufungua mkutano wa utalii Arusha Leo

Na Queen Lema ARUSHA

Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan anatarajia kufungua mkutano wa kimataifa wa 65 wa shirika la utalii duniani(UNWTO) Oktoba 5,2022.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha,Waziri wa maliasili na utalii,Balozi 

alisema mkutano huo unatarajia kukutanisha mawaziri wenye dhamana ya masuala ya utalii na maliasili kutoka nchi wanachama wa UNWTO wa kanda zaidi ya 50 kujadili kuhusu mustakabali wa ustawi wa maendeleo ya sekta ya utalii barani Afrika hasa baada ya athari za mlipuko wa janga la Uviko 19.

Aidha alibainisha kuwa  Uviko 19 umeathiri utalii wa kimataifa kwa wastani wa kati ya asilimia 50 hadi 85 katika nchi mbalimbali ikiwemo nchi yetu ya  Tanzania .

Dkt.Chana alisema mkutano huo utakuwa chachu ya kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo wataalam wa utalii na ukarimu katika ngazi ya kimataifa na kikanda,watoa huduma kwenye mnyororo wa utalii,wawekezaji pamoja na watu mashuhuri zaidi ya 150.

Alisema kuwa mbali na Rais Samia kufungua mkutano huo pia utahudhuriwa na Katibu mkuu wa shirika la UNWTO,Zurab Pololikashvili ambapo alibainisha kuwa  pia  patakuwepo na  matukio mbalimbali kama jukwaa la uwekezaji kwa ajili ya kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo nchini itazinduliwa Investment Guideline(Tourism Doing Business) sambamba na Marketing Symposium kwa ajili ya kuwajengea uwezo wadau wa utalii kuhusu masuala ya masoko.

Alisema kutakuwepo na uzinduzi wa A tour ofa African Gastronomy pamoja na ziara za mafunzo(FAM Trips) ambapo watapata nafasi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania ikiwemo Hifadhi ya Ngorongoro,Jumuiya ya wanyama pori ya Buruge na city Tour ya vivutio mbalimbali katika jiji la kitalii la Arusha,”alisema.

Alibainisha kuwa kulingana na sera ya Taifa ya utalii ya mwaka 1999 mkutano huo ni muhimu kwa kuwa ni mojawapo ya jitihada za serikali katika kuongeza idadi ya watalii nchini pamoja na kutanua wigo wa mazao ya utalii nchini kupitia uendelezaji wa mazao ya utalii kimkakati hususani utalii wa mikutano.

Vilevile alisema kuwa mkutano huo utawezesha kujengea uwezo wataalam wao na wadau wa utalii katika kutangaza utalii,kuendeleza na kufungamanisha mazao ya utalii katika kanda mbalimbali za utalii nchini kulingana na shabaha yao ya kuongeza idadi ya watalii milioni tano na mapato ya dola za marekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.

Waziri Chana alisema Mkutano umebebwa na kauli mbiu isemayo Rebuilding Africa’s Tourism Resilience for inclusive socio Economic Development huku aliongeza kuwa hii ni  fursa adhimu ya kukuza uchumi wa jiji la Arusha ,mikoa ya jirani na Tanzania kwa ujumla hivyo anatoa rai kwa wananchi katika kuchangamkia fursa zitakazotokana na mkutano