Rc mndeme akabidhi mwenge wa uhuru mkoani geita

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amesema miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri sita za Mkoa wa Shinyanga imezinduliwa, kufunguliwa na kuwekwa mawe ya msingi na Mwenge wa uhuru Mwaka 2023.

Amebainisha hayo leo Agost 2.2023 wakati akikabidhi Mwenge wa uhuru kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Martine Reuben Shigela

Amesema Mwenge wa uhuru umekimbizwa umbali wa kilomita 571.5 na kuona, kuweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua  jumla ya miradi 41 yenye thamani ya shilingi bilioni 14.27 katika Mkoa wa Shinyanga.

Miradi 11 yenye thamani ya shilingi bilioni 7.8 imewekewa mawe ya msingi, miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 3.3 imezinduliwa, miradi 4 yenye thamani ya shilingi bilioni 1.3 imefunguliwa huku miradi 12 yenye thamani ya shilingi bilioni bilioni 1.5 imeonwa.

Mwenge wa uhuru kwa Mwaka 2023 unaendelea kukimbizwa katika mikoa mbalimbali Nchini ukiongozwa na Bwana Abdalla Shaim Kaim pamoja na kaulimbiu inayosema tunza mazingira, okoa vyanzo vya maji kwa ustawi wa viumbe hai na uchumi wa Taifa.