Mbunge wa chadema joseph mbilinyi ‘sugu’ afunga ndoa


Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu leo Jumamosi Agosti 31, 2019 amefunga ndoa na Happiness Msonga katika Kanisa Katoliki Ruanda jijini Mbeya.

Katika misa hiyo wabunge 10 wa Chadema walihudhuria wakiongozwa na Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Silinde.

Wabunge hao ni Frank Mwakajoka (Tunduma); Anthony Komu (Moshi Vijijini); Lucia Mlowe, Sophia Mwakagenda na Lucy Mollel (wote Viti Maalum).

Wengine ni Joseph Haule (Mikumi); Joseph Selasini (Rombo); David Silinde (Momba); Pascal Haonga (Mbozi) na Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini).

Viongozi wa Chadema walioshiriki misa hiyo ni mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Sadick Malila na katibu wake, Emmanuel Masonga.