Rwanda yajiweka kwenye tahadhari kubwa kukabiliana na nzige….hadi sasa wametafuna hekta 70,000 za mashamba kenya, somalia na ethiopia

Rwanda
iko kwenye tahadhari ya hali ya juu kufuatia uvamizi wa nzige unaoweza
kutokea ambao kwa sasa wameonekana katika nchi kadhaa za Afrika
Mashariki, zikiwemo Ethiopia, Kenya na Somalia. 

Waziri
wa kilimo na rasilimali ya wanyama wa Rwanda Bibi Geraldine Mukeshimana
amesema, wizara yake iko tayari kukabiliana na uvamizi huo wa nzige. 

Shirika
la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa limesema, nzige wameharibu
karibu hekta 70,000 za mashamba nchini Somali na Ethiopia, na kutishia
utoaji wa chakula katika nchi hizo.