Serikali kuanza operesheni ujenzi madarasa 8000

 OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa Nchi nzima kuanza maandalizi ya oparesheni ya ujenzi wa Mdarasa Mpya 8,000 kwa ajili ya wanafunzi wanaomaliza darasa la saba na kujiunga na Kidato cha kwanza mwakani 2023.


Bashungwa ameyasema hayo  leo Septemba 24, 2022 jijini Arusha wakati akitoa taarifa kwa umma na vyombo vya habari kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Elimu nchini.


Amesema Muda wowote kuanzia sasa kabla ya mwezi huu kuisha pochi la Mama  Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan litafunguka kuwezesha oparesheni ya ujenzi wa mdarasa mapya 8,000 nchi nzima.


Bashungwa amesema oparesheni ya ujenzi wa mdarasa hayo itatumia mfumo uliotumika katika  ujenzi wa madarasa 15,000  kwa kuunda kamati Maalum za ujenzi.