Taasisi ya teknolojia dar es salaam wafanya tamasha la afya “dit afya day”

 Na Mwandishi Wetu 


Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT)  leo Tarehe 10/7/2021 imefanya Tamasha la Afya ‘DIT AFYA DAY’ lililoambatana na michezo na burudani mbalimbali kwa lengo la kuboresha afya za wanafunzi na wafanyakazi wa Taasisi hiyo. 


Akizungumza wakati wa kufungua Tamasha hilo, Naibu mkuu wa Taasisi Utawala na Fedha Dkt. Janat Mohammed amesema Tamasha hilo ni moja ya miongozo ya Serikali inayowataka Viongozi kuhakikisha wanaboresha afya za wafanyakazi wao. 

“Tutakua na michezo, mazoezi pamoja na mada mbalimbali zinazohusiana na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza na ndio maana tumezialika Taasisi mbalimbali zinazotoa huduma za kiafya ili tujumuike nazo kwasababu kupitia madaktari wao tutapata ushauri pamoja na kupima afya zetu ” amesema Dkt. Janat 


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo wa DIT Bwana Denis Madaha amesema kuwa Tamasha hilo  limeambatana na Michezo Kama mpira wa miguu, mpira wa kikapu,  mpira wa wavu,  kuvuta kamba,  kukimbiza kuku, ridhaa kukimbia kwenye magunia pamoja na kula tunda aina ya Apple .

Tamasha hilo liliambatana na burudani kutoka Kwa Msanii wa Muziki wa kizazi kipya maarufu kama BABA LEVO na mgeni rasmi ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Mhe.  Omary Kumbilamoto.