Meneja wa kanda ya Kusini Bi. Amina Yasini (TBS) akitoa mafun
zo kwa wadau wa bidhaa ya nafaka na mafuta ya kula wilayani Songea, Ruvuma.
Bi.Amina aliwafahamisha washiriki hao kuwa mafunzo hayo ni
endelevu kwani TBS imeadhamiria kuwasaidia wadau kuhakikisha jamii
inapata bidhaa bora na alishauri wazalishaji wasio na Leseni ya TBS
kuanza utaratibu mara moja.
Afisa Tehama (TBS) Bi,Jesca Matemba
akitoa elimu ya jinsi ya kutuma maombi TBS kupitia mfumo kwa
wajasiriamali wa mafuta ya kula na nafaka katika eneo la majengo
wilayani Songea.
Mkaguzi wa TBS, Bw. Barnabas Jacob
akitoa elimu kuhusu madhara ya vipodozi vilivyopigwa marufuku kwa
wafanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania(TTCL) wilayani
Songea, Ruvuma.
TBS kanda ya kusini imeendesha
zoezi la usajili wa majengo ya chakula na vipodozi katika mikoa ya
Ruvuma,Mtwara na Lindi na kubaini uwepo wa bidhaa hafifu za vipodozi na
chakula sokoni zenye thamani ya shillingi millioni 12/= ambazo
zimeteketezwa.
TBS inatoa wito kwa wauzaji na watumiaji wa bidhaa hizo kununua
bidhaa zilizothibitishwa ubora wake na TBS na kuzingatia ukomo wa muda
wa matumizi wa bidhaa husika.
Mkaguzi wa TBS Bw. Barnabas Jacob
akitoa mafunzo kwa wasindikaji wajasiriamali wa nafaka na mafuta ya
alizeti wa eneo la Majengo wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma.
Bw. Barnabas amewafundisha washiriki hao umuhimu wa viwango
,matakwa ya Viwango na namna gani viwango vinaweza kuwasaidia kuzalisha
bidhaa bora ambazo zitaweza kuleta ushindani katika soko.