Trafiki shinyanga wakagua magari ya shule, wenye magari mabovu waonywa

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mkuu wa Polisi kikosi cha usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga mjini mrakibu msaidizi wa Polisi Dezidery Kaigwa amekagua magari zaidi ya 14 yanayotumika kubeba wanafunzi lengo ni kuhakikisha vyombo hivyo vinakuwa salama.

Kaigwa ambaye pia ni mkaguzi wa magari ametoa elimu kwa watumiaji wa hao wa vyombo vya moto ambao wamefika katika zoezi hilo ambapo amesema hatokubali kuona gari bovu linatumika kubeba wanafunzi  hali ambayo ambayo inahatarisha usalama wao wa maisha.

Katika ukaguzi wake mkuu huyo wa usalama Barabarani Wilaya ya Shinyanga mjini Kaigwa amebaini changamoto mbalimbali kwa magari hayo ambapo ametoa maelekezo kwa watumiaji wa vyombo hivyo kuhakikisha changamoto hizo wanazitatua haraka na kwamba January 21 Mwaka huu 2022 magari hayo yarudishwe kwa ajili ya kukaguliwa tena.

“Kwa wale ambao tumebaini kuwa kunachangamoto tumeelekeza tarehe 21 mwezi wa kwanza Mwaka huu 2022 vyombo hivyo viletwe kwenye kituo cha Polisi ili viweze kukaguliwa tena kwa kufanyiwa malekebisho”.

“Niwatoe wasi wasi wazazi wale wazazi wa watoto kwamba vyombo vya moto vimekaguliwa viko salama na vile ambavyo tumekuta kuna changamoto tumetoa maelekezo viende kurekebishwa” 

Amezitaja baadhi ya changamoto zilizoonekana kwa baadhi ya magari hayo kuwa ni pamoja na kukosa mikanda pamoja na ubovu wa City cover ambapo ametoa maelekezo kuwa kufikia tarehe 21 mwezi huu pasiwepo na changamoto hizo.

 

Kaigwa amesisitiza madereva wote wa Wilaya ya Shinyanga kueshimu vivuko vya watembea kwa miguu kwa kuwapa vipaumbele wanao vuka.

Kwa upande wake mkaguzi wa polisi Wilaya ya Shinyanga mjini Emmanuel Pallangyo amewasisitiza madereva na watumiaji wote wa vyombo vya moto kuendelea kufuata taratibu, sheria na kanuni za usalama Barabarani ikiwa ni pamoja na nakutoendesha kwa mwendo kasi  ili kupunguza ajali zisizo za lazima.

Aidha Pallangyo amesema ni muhimu madereva wote katika Wilaya ya Shinyanga kuzingatia maadili ya udereva 

“Cha msingi ni sisi madereva kufuata sheria vyombo vitakaguliwa vitasahishwa makosa hiyo siyo tatizo kubwa, tatizo letu ni kufuata maadili ya udereva lakini pia tuangalia kuwa tunababa wanafunzi hilo ni kundi ambalo ni muhimu sana ndani ya jamii na serikali yetu tuende mwendo ambao ni mdogo mwendo salama”.

Wakizungumza baadhi ya madereva waliofika kwenye ukaguzi huo wameshukuru kwa elimu waliyopewa na kwamba  wameahidi kwenda kuzishughulikia changamoto pamoja na maelekezo waliyopewa.