Tucta yapendekeza kima cha chini mshahara kiwe milioni moja

Katibu Mkuu wa shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (TUCTA), Henry Mkunda


Na Mwandishi Wetu, Dodoma

SHIRIKISHO la vyama vya wafanyakazi Nchini, (TUCTA)  amesema shirikisho hilo  
 linapendekeza kiwango cha kima cha chini cha mshahara kwa mwezi kiwe shilingi milioni moja na elfu kumi.



KATIBU Mkuu wa shirikisho hilo,  Hery Mkunda ameyasema hayo leo Mei Mosi, 2022 wakati wa hotuba yake kwa Rais,  Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe hizo za siku ya wafanyakazi ambayo yamefanyika kitaifa kwenye uwanja wa Jamhuri, jijini Dodoma.


Mkunda amesema licha ya Rais Samia  kuzitekeleza hoja mbalimbali za wafanyakazi ikiwemo punguzo la makato ya kodi, kupandisha madaraja, bado TUCTA inapendekeza kuongezewa mishahara walau shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini.


“Kauli yako ya 2021 ulisema ‘Mimi ni Mama, na Mama ni mlezi’, hivyo mama tuna imani na matarajio makubwa juu ya ile ahadi uliyotoa kuhusu kutupandishia mishahara wafanyakazi wote Tanzania,’ amesema Mkuda na kuongeza.
… Mishahara walau iwe shilingi milioni Moja na elfu kumi kama kima cha chini. TUCTA tunapendekeza, bila shaka hotuba yako leo itakuwa tiba sahihi”.