Tunataka kombe la dunia mwaka huu- waziri mchengerwa

 Na Chalila Kibuda, Michuzi TV


Waziri wa Michezo , Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa ameitaka Timu ya Wasichana ya Serengeti chini ya Miaka 17 kuhakikisha wanarudi na kombe katika michuano itakayoanza Oktoba nchini India.

Mchengerwa ameyasema hayo leo wakati wa Kuaga Timu Serengeti Chini ya Miaka 17 katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kwa udhamini wa wadau wana imani ya kupata ushindi wa kurudi na kombe.

Amesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha timu ya Taifa kwa mpira wa miguu kutokana na kuchoka kuwa kichwa cha mwenda wazimu.

Mchengerwa amesema kuwa timu U-17 ya wasichana inakwenda kuweka kambi nchini Uingereza ambapo kwa timu hiyo kwao ni kujifunza na kubadilisha mazingira kwa kwa serikali ni kupata matokeo chanya.

Shirika la bima la Taifa (NIC) limekabidhi bima ya Afya yenye thamani ya shilingi Milioni 40 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) kwa ajili ya bima ya kuwalinda wakiwa majanga watayopata wakiwa nje ya nchi na timu ya taifa ya Walemavu (Tembo Warriors National Team) wakati wakijiandaa kushiriki michuano ya kombe la Dunia.

Waziri wa Mchengerwa ameipongeza NIC kwa kuamua kushiriki kwa namna moja katika kusaidia timu hiyo kwenda kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Dunia.

Aidha amewataka wachezaji wakapambane na kuweza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo kwani uwepo wa bima hiyo itaweza kuwasaidia pindi wanapopata changamoto katika michezo waweze kusaidika kwa urahisi na kwa haraka.

Hata hivyo amewataka wachezaji hao kutanguliza uzalendo wa nchi yao kwa kuhakikisha wanapambana na kufanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Elirehema Doriye amesema kuwa kwa wale wachezaji watakaoumia kila wiki watakuwa wanapewa laki moja kwa kipindi ambacho amekaa mpaka kufikia milioni 10, hivyo amewataka wachezaji hao kupambana na wasiogope kuumia kwa timu zote.

Amesema timu hizo ikifanya vizuri na kufika hatua ya robo fainali, watazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 40, wakifika nusu fainali watawazawadia shilingi milioni 80 na wakifika hatua ya fainali watapatiwa milioni 100.

“Mnatakiwa mkapambana na kuhakikisha mnaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, mkafanye vizuri na msigope kuumia hata hivyo ikitokea mchezaji akapata kilema cha kudumu atalipwa hivyo basi NIC ipo kwaajili yenu na tunawatakia kila la heri kwenye michuano hiyo”. Amesema Dk..Doriye.

Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa akizungumza katika hafla ya kuaga Timu ya Wasichana ya Serengeti chini ya miaka 17 inayokwenda kushirika Kombe la Dunia nchini India katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza kuhusiana na Udhamini wa Timu za Taifa za Serengeti U-17 na Timu ya Walemavu zinazoshiriki Mashindano ya Dunia hivi karibuni wakati wa hafla ya kuiaga timu ya Serengeti U-17 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mohamed Mchengerwa akipokea hundi ya Sh.Milioni 40 kwa ajili ya majanga ya timu za Serengeti U-17 na Timu ya Walemavu kwa ajili ya kusaidia majanga mbalimbali wakiwa nje ya nchi  katika hafla ya kuaga Timu ya Wasichana ya Serengeti chini ya miaka 17 inayokwenda kushiriki  Kombe la Dunia nchini India  hafla hiyo  iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Timu ya Taifa ya Wasichana ya  Serengeti U-17 wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa akiambatana viongozi na watendaji wa Wizara hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wasichana ya  Serengeti U-17 wakisikiliza nondo za viongozi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *