Ubalozi wa ufaransa waandaa tamasha la marafiki

 Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam

KITUO cha utamaduni cha ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kimeandaa tamasha la marafiki ambapo jumla ya bendi 16 na wasanii 128 watatumbuiza kwenye tamasha hilo la marafiki 2021.


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye kituo cha utamaduni cha ufaransa Allience francases mratibu wa tamasha hilo Isack Abeneko alisema marafiki ni tamasha la mziki la kimataifa ambalo huwaleta pamoja wasanii.

Alisema katika tamasha hilo wasanii wa ndani na wakimataifa watapata fursa ya kuonyesha mziki wao ambapo Pamoja na mambo mengine tamasha hilo litawaleta wadau pamoja na watalaamu mbaalimbali wasanaa na watashiriki pamoja na kubadilishana uzoefu.

“lengo la tamasha hili la marafiki nikuwajengea uwezo wasanii katika maeneo mbalimbali ya sanaa zao .tamasha la marafiki linatarajia kukuleta muziki mzuri wa moja kwa moja na maarifa kwa wakati mmoja kuazia oktoba 7,hadi 9 ambapo pia kutakuwa na marafiki extra firefly bagamoyo oktoba 10.2021.”alisema Abeneko

Nakuongeza kuwa “kauli mbiu ya tamasha hilo ni Muziki wa maendeleo ya jamii” kuhamasisha vijana na wanamuziki kutumia muziki kama nyezo ya kuleta mabadikiko chanya ya kijamiii.

Pia tamasha la marafiki litakuwa na semina za mafunzo na mijadala ya wazi kwa siku tatu ambapo mada kama uratibu wa biashara ya muziki, utengenezaji wa muziki kwenye mzunguko na unaofaa kwenye usimamizi wa wasanii, jinsi ya kupata shoo katika soko la ndani na la kimataifa. Pamoja na jinsi ya Luanda epk zote zitawasilishwa.

Alisema mjadala wa wazi ukuwa juu ya biashara ya muziki na jinsi ya kuufanya muziki wa afro -fusion uwe muhimu na utumike ndani ya soko la Tanzania na afrika mashariiki nakwamba washa zitaaza saa 04:00 asubuhi 07 mchana siku zote tatu na zitafanyika Nafasi art space na Alliance Francaise .upanga Dar es salaam..