Ujerumani: marekani imeshindwa katika makabiliano yake na iran

Waziri
wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas amekosoa sera za rais Donald
Trump wa Marekani za kuongeza shinikizo dhidi ya Iran. 


Maas
ameliambia gazeti la Ujerumani la Bild am Sonntag kwamba hawapaswi
kudhania kwamba shinikizo kutoka nje dhidi ya Iran litaweza kuimarisha
hali ilivyo nchini humo na kuongeza kuwa hatua kama hiyo ilikuwa na
matokeo mabaya katika nchi kama Iraq. 

Maas amesema vitisho dhahiri pamoja na hatua za kijeshi na vitisho havijaweza kubadilisha tabia za kiuongozi za Tehran. 

Chama
cha Social Democrat, SPD kimesisitiza kwamba mazungumzo ni njia muhimu
itakayosaidia kupiga hatua na kuimarisha sera ya Ulaya kuelekea taifa
hilo.