Uvccm st. joseph mbezi wavunja rekodi hii kubwa

Jumamosi ya  29 May 2021 UVCCM Tawi la Chuo kikuu Cha St Joseph Mbezi Campus  walifanya darasa la itikadi liliohudhuriwa na wanachama mbalimbali.


Darasa hilo la itikadi lilifanyika katika ukumbi wa Big C magari saba, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Comred ALLY M UMMY katibu wa uhamasishaji na chipukizi Mkoa wa Dar Es Salaaa.


Mgeni rasmi ndg ALLY UMMY kabla ya kufika ukumbini aliingia chuoni na kuangalia projects zilizoandaliwa na wanafunzi wa uhandisi ambazo zilikuwa ni za kibunifu zaidi.


Katika darasa la itikadi Mgeni rasmi alijikita kueleza juu ya historia ya Chama chetu lakini pia alieleza zaidi juu ya elimu ya ujamaa na kujitegemea.


Mwisho ndugu mgeni rasmi aliupongeza  Uongozi wa UVCCM Chuo kikuu Cha St Joseph  kwa kuandaa darasa la itikadi la kibunifu zaidi, lakini pia aliupongeza Umoja wa vijana wa CCM St Joseph kwa kuwa na mahusiano ya karibu na vyuo vingine pamoja na uongozi wa CCM kata ya kwembe na wilaya ya UBUNGO.


Hali kadhalika ndg ALLY UMMY aliupongeza Umoja wa vijana wa CCM  St Joseph University kwa kuchangia madawati mawili ambayo yalikwenda kusaidia shule ya king’azi A iliyopo Mbezi ambayo ilikuwa na  uhaba wa madawati kwa lengo la kuiunga mkono serikali ya JMT

 

Imetolewa na 

 BARAKA M KAGOMA 

Katibu wa UVCCM Tawi la Chuo kikuu Cha St Joseph Mbezi campasi@ 0678216613