Vijana watakiwa wajiunge na jeshi badala ya kukaa vijiweni

Mkuu wa wilaya ya Arusha Musa Mtanda kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa jeshi la akiba

 Na Queen Lema Arusha

Vijana wasio na ajira wametakiwa kuachana na tabia ya kukaa vijiweni na kupiga hadithi ambazo haziwasaiidi na badala yake muda huo watumie kujiunga na majeshi ya akiba ambayo mafunzo yake huwafanya waweze kupata ajira kwa uraisi sana 

Kwa Sasa Kuna dhana kuwa vijana waliojiunga na majeshi ya akiba wamejiunga tu ili waweze kuajiriwa kwa ajili ya kuwasumbua machinga jambo ambalo sio la kweli kwa kuwa askari wa jeshinla akiba ni askari kama walivyo askari wengine

Hayo yameelezwa na mkuu wa wilaya ya Arusha Musa Mtanda wakati akifunga rasmi mafunzo ya Jeshinla akiba kwa Jiji la Arusha pamoja na maafali Yao ya 46 mapema jana kwenye viwanja vya Gymkana Arusha 

Mtanda alisema kuwa kujiunga na jeshi la akiba sio ushamba Bali ni nafasi pekee ya kujitengenezea fursa hasa ya ajira kutoka serikalini au sekta binafsi hasa za ulinzi 

Aliongeza kuwa kwa Sasa kijana ambaye amepitia kwenye mafunzo ya jeshi la akiba fursa za kujiunga na majeshi mengine zinapotokeaa inakuwa ni raisi sana kuweza kupata nafasi lakini kwenye jamii nayo ni raisi sana kuweza kupata anira hasa katika makampuni ya ulinzi

Alifafanua kuwa ni wakati Sasa wa vijana kuachana na tabia ya kukaa katika magenge na kuja katika mafunzo hayo ya jeshi la akiba kwa kuwa ni fursa

“Sikia niwaambieni ni hivi unakuta mtu mzazi wake amemsomesha kuanzia ngazi ya chini hadi kufukia chuo kikuu na hajapata ajira Sasa anaona kuliko ajiunge na jeshi la akiba ni Bora akae tu mtaani nawaambia kuwa mnakosea sana sana,msidharau hili jeshi la akiba hata siku moja”aliongeza.

Naye mshauri  wa mgambo kutoka jiji la Arusha Meja Hija Khamisi alisema kuwa vijana waliohitimu wamepata mafunzo kwa muda wa miezi minne na nusu na wameiva kwa ajili ya kulitumikia taifa 

Alisema kuwa vijana hao walikuwa 138 pindi walipoanza masomo Yao lakni waliofanikiwa kuhitimu ni 118 pekee na hao wengine waliacha kwa sababu mbalimbali ikiwemo kwenda kujiunga na majeshi mengine 

Meja Hija alitoa wito kwa vijana hasa wa kike kuhakikisha kuwa wanajitokeza kwa wingi hasa wanaposikia nafasi zimetangazwa kwa kuwa jeshi la akiba huwa lina fursa nyingi sana za ajira kwa Sasa.

“Watoto wa kike hawatakiwi kuogopa na wasiwe na hofu,idadi hata ya waliohitimu siku ya Leo ni ndogo sana,nawasihi sana waje tu wajitengenezee nafasi za kwenda juu zaidi”aliongeza

Naye Bw Victor  Gaudence  ambaye ni meneja wa kampuni ya ulinzi ya SGA akiongea kwa niaba ya wamiliki wa kampuni za ulinzi kwa mkoa wa Arusha aliwasihi sana vijana kuachana na tabia ya kudharau jeshi la akiba kwani kupitia jeshi Hilo ajira nyingi sana zimeweza kuibuliwa.

“Mimi kwa Sasa ni meneja wa kampuni kubwa sana ya ulinzi hapa nchini lakini nataka niseme nami pia nimepita hapa hapa kwenye uwanja huu huu na nilifanya kazi yangu kwa uhaminifu mkubwa sana na kila mara nikawa napanda mpaka kufika hapa ningeipuuza hilo jeshi nisingefika hapa nawapenda kuwaambia vijana wasijidharau au kuogopa kujitangaza kuwa ni wahitimu wa mafunzo kutoka jeshi la akiba”aliongeza 

Katika hatua nyingine alisema kuwa kampuni ya SGA Sasa itawachukua wahitimu hao na kisha kuwapa ajira rasmi hasa kwa wale ambao watakuwa na vigezo ili vijana hao waweze kulitumikia taifa kwa upana zaidi na kuachana na tabia ya kujihesabu kama Hawana ajira.