Vyama13 vyajitokeza kuwania ubunge ngorongoro, ni kufuatia kifo cha ole nasha

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ngorongoro, Juma Mhina akikabidhi mgombea wa CCM timu ya kuwania nafasi hiyo baada mgombea huyo kupitishwa na chama chake

 Ngorongoro, Novemba 11,2021

Na Mwandishi Wetu

WAGOMBEA wa vyama  13 vya Siasa wamejitokeza kuwania  ubunge katika jimbo la Ngorongoro  katika uchaguzi mdogo unatarajiwa kufanyika Disemba 11 mwaka huu.

Uchaguzi huo mdogo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Willium Ole Nasha kufariki Septemba 27 mwaka huu Jijini Dodoma muda mfupi baada ya kurejea kutoka Jijini Arusha kikazi.

Kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Ngorongoro Dk,,Juma Mhina ametaja wagombea hao kuwa ni  pamoja na 

Emmanuel Shangai (CCM)  Simon Bayo (SAU) Singa Kalekwa (CCK), Amina Mcheka (NLD) Mary Daudi (UPDP).

Amewataja  wagombea wengine kuwa ni Mgina  Mustafa (AAFP),.Frida  Nnko  (UMD),Paulo  Makuru (UDP),Shafii Kitundu (ADC), Feruziy Feruziyson (NRA),

Simon P Ngilisho (DEMOKRASIA MAKINI), Jonson  Gagu (ACT WAZALENDO) na  Zuberi Hamis (ADA TADEA).

“Zoezi la utoaji wa fomu lilianza Novemba 9 mwaka huu na mpaka Novemba 11 mwaka huu wagombea 13  kutoka  vyama mbalimbali  vya siasa  hapa nchini wamejitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kujaza nafasi hiyo ya  ubunge”.

Amesema   NEC itaendelea kutoa fomu hizo hadi Novemba 15 mwaka huu saa 10:00 jioni  na wagombea na siku hiyo hiyo watatafanya uteuzi wa wagombea ambao watakuwa wamekidhi sifa za  kugombea ubunge wa jimbo hilo.

“Wagombea wote watatakiwa kurejesha fomu zao Novemba 15 mwaka huu na endpo kuna mgombea yeyote atakayepata changamoto wakati wa kujaza fomu yake ofisi zetu  za NEC zitakuwa wazi muda wote kwa ajili ya kutoa msaada kwa wagombea ikiwa ni pamoja na uhakiki iwapo fomu zimejazwa vizuri kabla ya kuzirejesha”.

Amesema baada ya uteuzi utakaofanyika  November  15 mwaka huu  wagombea watakopitishwa kushiriki uchaguzi  huo wataanza kampeni Novemba 16 hadi Disemba 10 mwaka huu na uchaguzi utafanyika Disemba 11 mwaka huu.