Na Mwandishi Wetu, APC BLOG, DODOMA
WASHIRIKI wa kundi kazi namba 3 la mafunzo ya Vyombo vya Habari mbadala (Alternative Media) chini ya ufadhili wa Mradi wa Ushawishi kwa kutumia takwimu (Data Driven Advocacy DDA) wametakiwa kujitafakari na kutimiza wajibu wao.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu alipofungua mafunzo ya Haki za Binadamu leo mjini Dodoma yanayoratibiwa na Shirikisho la Vyama vya Waandishi wa Habari nchini (UTPC).
“Washiriki wa “Work Group Three” tutimize wajibu wetu kwa yaliyo ndani ya uwezo wetu, bado hatujaona habari za haki za binadamu na demokrasi kama ambavyo tunatakiwa kufanya.
“Tunaendelea kufuatilia kwa makini namna gani tutapunguza washiriki katika kundi hili, wafadhili wetu wameendelea kujiuliza na kuhoji kuhusu mafunzo tunayopewa na wajibu wetu,” amesema Gwandu.
Katika hotuba yake Gwandu aliwataka washiriki hao kuwa na matumizi mazuri ya muda wa kujifunza na kumsikiliza mwezeshaji badala ya kujikita kutumia Laptop na simu wakati wa mafunzo.
“Nyinyi ni watu wazima mjitathimini mmesafiri kutoka makwenu kuja kushiriki mafunzo yanayogharamiwa kwa fedha nyingi, haipendezi kuona mshiriki akitumia muda mwingi kwenye laptop yake na kucheza game kwenye simu.
“Hili ni darasa la watu wazima na wabobezi tumekuja kujifunza na kubadilishana uzoefu, tunaweza kuzima Laptop zetu na kumsikiliza mwalimu.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC) Claud Gwandu wakati akifungua mafunzo ya Haki za Binadamu mjini Dodoma yaliyoshirikisha waandishi wa habari mtandaoni (Blogs/Online Tv ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Utetezi na Ushawishi wa Haki za Binadamu kwa kutumia takwimu (DDA) kupitia vyombo vya habari mbadala (Alternative Media). Picha zote na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Froldius Mutungi akitoa mada kuhusu haki za binadamu.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Haki za binadamu Wakili Froldius Mutungi akitoa mada kuhusu haki za binadamu.