Mbowe atema cheche arusha

 Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo  taifa Freeman Mbowe amemtaka Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan Kutoruhusu sera za kisiasa za kuwagawa watu kwa njia ya ukabila na badala yake kujenga taifa lenye misingi ya kuheshimu haki na usawa kwa watu wote.


Kwa muktadha huo kuacha kupendelea Watanzania na badala yake kila Mtanzania apewe fursa ya Haki inayostahi kufaidi Keki ya Taifa lao na kwamba uongozi wa  nchi usitolewe kwa misingi ya upendeleo wa Kikabila na badala yake uongozi utolewe kwa misingi ya mtu kuwa na sifa uwezo wa uongozi.

Alisema serikali itakayoongozwa na chama hicho itafuta suala zima la ukabila kwenye Fomu za maombi yoyote ili kuweka utanzania mbele kwa maslahi ya Taifa letu ikiwemo kuondoa ubaguzi wowote nchini.

Ameendelea kumtaka mama Samia Suluhu Hassan kutengeneza Amani na suluhu katika Taifa hili kwani mioyo ya watu inavuja damu na kwamba wasione aibu kuomba radhi pale mlipowakosea watu na kutambua ndani ya serikali yako wapo mawakala walitumika kwenye ukatili .

“Tunasikia kauli zako za kurejesha matumaini  lakini haitoshi kwa miaka mitano mlitumia kanuni sheria za kuminya haki na uhuru wa vyombo vya habari haki ya vyma vya siasa na Demokrasia haki za kibiashara na kuwatesa wafanyabiashara kupitia kodi ikiwa ni kinyume cha haki za binadamu”

Ameeleza kuwa chama hicho hakiwezi kuwa chama cha visasi japo watu wengi wameifanyiwa matukio mengi na lazima watumie mbinu kurudisha haki kwa kujali utu kwa Watanzania.

Amewataka viongozi wan a wanasiasa kuhakikisha wanaresha utengamano wa taifa letu kwa kuongoza mapambano ya kurejesha haki utawala wa kisheria na kikatiba  katika Taifa letu.
Aidha alieleza kuwa viongozi wa chama hicho kuelekeza mapambano katika kuwaeleza wananchi juu ya kuwaonya viongozi wa taifa letu bila kujali itikadi zao kuhakikisha wanaongoza taifa hili kwa misingi ya sheria kanuni na kikatiba.

Alikemea vikali kutoruhusu kauli za watawala kuwa sheria na watawala kuwa na umungu watu,na kutoruhusu watawala wanaoweza kuchezea Bunge na Mahakama zetu pia tusiruhusu taasisi za umma kuchezewa kama vipandia vya kutekeleza matakwa ya viongozi ambayo ni kinyume cha sheria na katiba ya Taifa letu.

Alisema jambo hili ni jukumu letu na linapaswa kubebwa na wananchi wote ili kurudisha maridhiano ya taifa bila kuangalia maumivu tuliyopitia kama taifa kwa kipindi cha miaka mitano na wala tusiwe watu wa visasi bali tuelekeze nguvu zetu kudai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
“Siku zote nimewaonya wanachedema  kutobeba visasi katika mioyo yao kwani hiyo ni kazi ya Mungu na kuelekeza taifa kwenye misingi ya kudai haki kwa wananchi ikiwemo Katiba yenye kujali usawa na utu wa Watanzania”

Amebainisha kuwa chama hicho kimejipanga katika misingi ya kudai haki na wao wamejipanga kukirudisha chama ngazi ya chini kabisa kwenye mioyo kwa lengo la kulikomboa taifa letu.

Pia chama hicho kimezindua mtandao wa kusajili wananchama kwa njia ya kidigitali kwa lengo la kukiimarisha na kuongeza mapoto yatakayosaidia kujenga makao makuu ya chama hicho nchini na kanda zote.

Mwisho