Wakazi wa mabambasi waliomba tanesco kudhibiti vishoka

 Na Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Mabambasi Kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga wamelitaka Shirika la umeme Tanzania TANESCO Mkoa wa Shinyanga kuchukua hatua za haraka kudhibiti wimbi la watu matapeli wanaopita Mitaani na kujitambulisha kuwa ni watumishi wa Shirika hilo

Wamesema  kuwa hali hiyo imetokea hivi karibuni baada ya watu waliofika katika baadhi ya nyumba zinazohitaji,  huduma ya kufungiwa umeme  kujitambilisha kuwa wao wametumwa na shirika la umeme TANESCO ambapo bila shaka yoyote wananchi hao waliwapa ushirikiano ikiwa pamoja na kulipia gharama za huduma hiyo 

Wananchi hao wamedai kuwa baada ya kulipia gharama hizo walisubiri kuletewa huduma lakini haikufanyika hivyo hali iliyowalazimu kufuatilia kwenye ofisi za TANESCO zilizopo Mjini Shinyanga, lakini waliambiwa kwamba Shirika halina taarifa za watu hao hali ambayo imewashangaza na kusema kuwa kama isipotafutiwa ufumbuzi wa haraka itawaondolea  imani dhidi ya Shirika hilo     

Wananchi hao pia wamelalamikia  kucheleweshewa kufungiwa huduma ya umeme licha kukamilisha hatua na taratibu zote zinazohitajika, lakina wamekuwa wakizungushwa kila wakati bila kupewa sababu za msingi 

Kaimu meneja  wa shirika la TANESCO Mkoa wa  Shinyanga, Mhandisi BERNARD MAJURA ameeleza kuwa shirika limechukua hatua za haraka kufanya uchunguzi juu ya tuhuma hizo, ili kubaini kiini cha tatizo hilo

Kuhusu malalamiko ya kucheleweshewa huduma Injinia MAJURA amesema Shirika litashughulikia changamoto ya wananchi hao ambapo pia amewaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza akidai kuwa hali hiyo inachangiwa na kuelemewa na wateja wengi wanaohitaji huduma hiyo

“Niwaombe radhi wateja kwa kuchelewa kuwafikia maana tulipaswa kuwafikia kwa muda muafaka lakini tumechelewa kwa idadi kubwa ya watu”

“Wateja ni wengi wenye changamoto kama hizo na tumekuwa tukiwafikia kwa maeneo tofauti tofauti kwa sababu tumeanzia maeneo yenye wateja wengi tutamalizia na maeneo yenye wateja wachache lakini tunaimani wateja wote tutawafikia wawe na imani na shirika letu kwamba watapata huduma”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *