Wanafunzi 14 wafariki kwa kukanyagana kenya

Wanafunzi
14 wamefariki dunia huku wengine 39 wakijeruhiwa katika Shule ya Msingi
Kakamega nchini Kenya kutokana na kukanyagwa na wenzao na kuanguka
wakati wakikimbia.


Ajali
hiyo imetokea Jumatatu Februari 3 majira ya saa 11 joni wakati watoto
hao wakitoka madarasani kurejea makwao, ambapo tayari wanafunzi 20
waliojeruhiwa wameruhusiwa kutoka hospitali.

“Kumpoteza
mtoto ni tukio linalouma sana. Natoa salamu za pole kwa wazazi wote
waliofiwa na watoto wao,” Waziri wa Elimu, George Magoha amesema.

Kamanda
wa Polisi wa Kakamega, David Kabena amesema chanzo cha tukio hilo
hakijafahamika lakini amebainisha kuwa tayari uchunguzi umeanza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *