Wananchi shinyanga waipa kongole shuwasa

 


 Na Mapuli Misalaba,
Shinyanga

Kuelekea kilele cha
maadhimisho ya siku ya Maji Duniani baadhi ya wananchi katika Manispaa ya
Shinyanga wamepongeza huduma zinazoendelea kutolewa na Mamlaka ya maji safi na
usafi wa mazingira  Manispaa hiyo SHUWASA
huku wakitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili.

Wananchi hao wametoa
pongezi hizo  leo wakati wakizungumza na Misalaba
Blog kwa nyakati tofauti kuelekea maadhimisho hayo.

Wamesema kuwa wanaendelea
kupata huduma ya maji lakini bado zipo changamoto zinazohitaji ufumbuzi ili
kuwasaidia wananchi kuendelea kunufaika na huduma hiyo na kwamba wameiomba
Mamlaka hiyo kuboresha zaidi huduma ya maji safi na salama kwa wananchi sambamba
na  kutatua changamoto ya  bili za maji.

Kwa upande wake  Afisa Mahusiano na mawasiliano kutoka Mamlaka
ya maji safi na usafi wa mazingira Manispaa ya Shinyanga SHUWASA, Bi Nsianeli
Gerald amewataka  watumiaji wa huduma hiyo
kutoa taarifa pale  inapotokea changamoto
ili ishughulikiwe haraka.

Akizungumzia siku ya maji
Duniani Bi Nsianeli amesema mamlaka hiyo tayari imefuta faini za wateja
waliokatiwa maji na badala yake watalazimika kulipa madeni yao kwa makubaliano.

Kesho ni kilele cha
maadhimisho ya wiki ya maji Duniani ambayo ilizinduliwa rasmi Machi 16, Mwaka
huu ikiongozwa na kaulimbiu inayosema “kuongeza
kasi ya mabadiliko katika sekta ya maji kwa maendeleo endelevu ya uchumi
”.