Aliyeiba chupi 100 za wanawake tofauti tofauti akutwa amevaa mbili

Mwanaume mmoja mwenye tabia ya Wizi wa nguo za ndani za wanawake,
anayejulikana kwa jina la Mukoshi Chipukosia (36), kutoka kijiji cha
Hirumbi nchini Kenya, amekamatwa na kufikishwa kwa Mjumbe wa Nyumba Kumi
kwa kosa la kuwaibia wanawake nguo za ndani ‘chupi’ 100 na kukutwa
amevaa mbili.
Kwa mujibu wa Mjumbe wa Nyumba Kumi amesema, mwizi huyo amekutwa
hadharani akiwa amevaa nguo hizo, wakati anajaribu kuiba zingine kwenye
kamba na ndipo Mbwa wa ulinzi wa eneo hilo akaanza kubweka na kumshtua
mmiliki.
Aidha mmoja wa wamiliki wa nguo hizo amesema, alikuwa anachunga Ng’ombe
ghafla akasikia Mbwa wake anabweka na alipoenda akamkuta mwizi huyo
anaiba.
“Tumechoshwa na hii tabia, anachofanya sio tabia nzuri, anaiba nguo za
ndani za wanawake pekee, kwanini isiwe na za wanaume, kila mara
anatuibia sisi tu inatushangaza ni aina gani ya wizi huu bora angeiba
Kuku, Mbuzi au Ng’ombe ila sio nguo za ndani imetushtua sana” amesema
mmoja wa waathirika wa wizi huo.
Pia mwizi huyo amejitetea kwa kusema yeye ni maskini, hana pesa za
kununua nguo za ndani za kiume kwa hiyo ilikuwa inamlazimu kuiba na
kuahidi kuwa hatorudia tena.
Chanzo ni Tuko News na K24 Tv.