Aliyeua mke wake kwa shoka akamatwa arusha

Jeshi
la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kumkamata muimba kwaya Moses
Pallangyo (28), aliyemuua mke wake Mary Mushi, kwa kumkata na shoka
kichwani, katika kijiji cha Kilinga wilayani Arumeru na kwamba baada ya
mahojiano, mtuhumiwa huyo amekiri kufanya mauaji hayo.


Akizungumza
leo Disemba 29, 2019, Kamanda wa Polisi mkoani humo Jonathan Shanna,
amesema kuwa jeshi hilo lilimsaka mhalifu huyo kwa kutumia kikosi cha
Mbwa ambacho ndicho kilichofanikisha kumkamata, akiwa mafichoni kuelekea
nchini Kenya.

“Jana
Disemba 28 saa 11: 30 jioni, tumefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo,
ambaye tuliahidi kumtafuta kwa namna yoyote ile na ‘Dog Style’ ndiyo
imeleta mafanikio ya kumkamata yaani ilikuwa bandika bandua, mtuhumiwa
tumemhoji kwa kina na amekiri kufanya kitendo hicho cha kikatili, na
tulitaka kujua kwanini amefanya kitendo hicho akasema ni shetani
alimpitia” amesema Kamanda Shanna.

Tukio
hilo lilitokea Disemba 25, 2019 majira ya mchana, jambo ambalo hapo
awali lilihusishwa na ugomvi wa kifamilia ikiwemo wivu wa mapenzi.