Amuua mama yake na kunywa damu

Kamanda wa Polisi Arusha ajibu mapigo, 'Kaangalieni Katiba ya CCM ...
Kamanda wa Polisi Arusha Jonathan Shana
JESHI la Polisi mkoa wa Arusha,linamshikilia Daniel Emauel, (32)  mkazi wa kijiji cha Sakila,kata ya King’ori, wilayani Arumeru, kwa tuhuma za kumuua mama yake mzazi,aitwae  Eliamulika Emanuel Salakikya(79) ambae ni mkulima mkazi wa kijiji hicho cha Sakila,  kwa kumkata na shoka shingoni na miguuni na kutenganisha kichwa  kiwiliwili.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shana, amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3.00  na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Amesema kuwa mtuhumiwa ana matatizo ya akili kwani mara baada ya mauaji hayo alichukua chombo na kukinga damu ya marehemu na kuinywa.
Amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya mkoa ya Mount Meru.
Katika tukio lingine Moto uliozuka jana usiku wa kuamkia leo eneo la Sanawari jijini Arusha, umeteketeza nyumba na kusababisha kifo cha mtu mmoja Enock Joachim Asenga(17) muuza duka.
Moto huo uliwaka katika chumba cha biashara ambacho marehemu alikuwa amelala
Amesema marehemu alikuwa ameajiriwa na Deogratius Benedcti, (28) kuuza duka .
Amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la Zimamoto na uokoaji, pamoja na wananchi walifanikiwa kuzima moto huo na kutoa mwili wa marehemu  ukiwa umeungua vibaya.
Amesema bado wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo na hasara iliyopatikana ingawa taarifa za awali zinaeleza kwamba katika chumba hicho kulikuwa na mitungi ya gesi .
Mwili wa marehemu umehifadhiwa hospital ya mount meru  kwa ajili ya uchunguzi zaidi 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *