Askari polisi akatwa uume na mkewe shinyanga

Picha haihusiani na habari hapa chini

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog


Askari polisi aitwaye Kazimir (28) mkazi
wa Shinyanga Mjini amenusurika kifo baada ya sehemu zake za siri
kukatwa na kitu chenye ncha kali akiwa amelala na mkewe Flora Adam (23)
kutokana na kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi ‘mme kuwa na mchepuko’.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga Deborah Magiligimba amesema
tukio hilo limetokea Desemba 28,2019 majira ya saa 6 na nusu usiku
wakati wamelala ambapo ghafla alikatwa na kitu chenye ncha kali katika
sehemu ya uume wake. 
“Wakiwa wamelala mke wake Frola Adam aliamka na kunyatia na kuchukua
kitu chenye ncha kali na kumkata mmewe kwenye sehemu zake za siri na
kumjeruhi vibaya na kumsababishia maumivu makali”,
amesema Kamanda Magiligimba. 
“Baada ya tukio hilo Pc Kazimir alikimbizwa katika Hospitali ya rufaa
ya Serikali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa siku mbili na
badaye aliruhusiwa”
,ameeleza. 
Amesema chanzo tukio hilo kuwa ni wivu wa kimapenzi jambo linalosadikiwa kwamba mme wake alikuwa na nyumba ndogo.  
“Tunamshikilia Frola Adam (23) kwa tuhuma ya kumkata mume wake
sehemu za siri na baada uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani
kujibu tuhuma zinazomkabili”
,amesema Kamanda Magiligimba.