Na Ahmed Mahmoud Arusha
Halmshauri ya Jiji la Arusha imeendelea kusimamia sheria za ulimaji wa mahindi na mifugo kwa maeneo ya katikati ya Jiji Ila nje ya mji bado sheria hiyo haijafika huko mfano Kata ya Teret.
Aidha Baraza hilo likataka Taarifa za mikopo ilivyotolewa na fedha zilizorejeshwa na kuainishwa vikundi na kundi maalumu walionufaika na mikopo ya vijana na kinamama.
Akiongea kwenye kikao hicho Diwani wa kata ya Muriet Mbise alisema taarifa hiyo ipo sawa hivyo waendelee na mjadala mwingine Ila waongeze ufanisi kuwafikia kada hiyo.
Baraza hilo likaendelea na maswali na majibu ambapo Diwani wa kata ya Kati Abdulrasul Tojo kutaka kujua maboresho ya masoko na mapato kwenye masoko ya Engutoto na Njiro.
Kwa upande wake kaimu Mstahiki meya Isaya Doita alisema kuwa sheria za mifugo na ulimaji wa mahindi zinahitajika kusimamiwa ipasavyo ili kuondoa changamoto ya kulifanya Jiji kuwa sehemu ya mashamba.
Ruzuku ya Tasaf imekuwa changamoto kutokana na kaya maskini kutolipwa kwa mwaka Jana mzima kutokana na usajili wa njia ya mtandao huku wazee hawajalipwa mkupuo huo wa fesi 1
Diwani wa Kata ya Kimandolu Gaudency Lyimo alitaja kujua kata za Moivaro na Terat lini watafanya upimaji wa maeneo kujua mipaka linalofanya kuendelea kuwepo kwa makazi holela.
Uwekezaji katika milima halmashauri imetenga kiasi cha milioni mia kwa ajili ya uwekezaji kwenye maeneo na wanaendelea kutafuta wawekezaji wa kushirikiana na halmashauri.
Baraza hilo linaendelea na kikao chake kwa kwa kupitia mjadala wa taarifa na muktasari wa kikao kilichopotia na maswali ya papo kwa papo kwa lengo.