Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya shinyanga laridhia kufukuzwa kazi watumishi wawili

Na Mapuli Kitina Misalaba

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya
Shinyanga limeridhia hoja ya kufukuzwa kazi watumishi wawili kwa makosa
mbalimbali ikiwemo utoro kazini .

Tamko la kufukuzwa kazi  watumishi hao limetolewa kwa niaba ya madiwani
leo Alhamis Machi 7,2024 na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nikodemus Luhende  kupitia mkutano wa Baraza hilo katika kipindi
cha robo ya pili ya Mwaka wa Fedha 20232024.

Watumishi hao ni ambao walikuwa wanatuhumiwa kwa
makosa ya utoro kazini, ubadhilifu na kufanya kazi kinyume na maadili ya
utumishi wa umma ni Mtendaji wa kijiji cha Mwanono kata ya Didia pamoja na
Afisa ustawi wa jamii Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Kilian Nestory Mlalama.

Azimio hilo la Madiwani, limefanyika baada ya
kuzingatiwa kwa taratibu zote za kisheria zinazotakiwa katika kuwawajibisha
watumishi wa Halmashauri.

Aidha katika mkutano wa Baraza hilo Madiwani pamoja
na viongozi wengine wamebainisha mambo mbalimbali ikiwemo changamoto za
miundombinu pamoja na Maji huku taarifa mbalimbali zikiwasilishwa.

Katika taarifa yake kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga Dkt. Nuru Hahya Yunge ameelezea zoezi la uandikishaji
wanafunzi wa awali na Darasa la kwanza pamoja na uandikishaji wanafunzi kidato
cha kwanza.

“Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga inajumla ya shule za awali na msingi 139 jumla ya
wanafunzi walioandikishwa wa Darasa la awali ni 11,325 kati yao Wavulana ni
6320 na Wasichana ni 50005 sawa na asilimia 70 ya wanafunzi 16,245
waliotarajiwa kuandikishwa lakini kati ya wanafunzi hao walioandikishwa 20
wameandikishwa kama wanafunzi wenye mahitaji maalum kati yao Wavulana 10 na
Wasichana 10”.

“Wanafunzi
wa Darasa la kwanza walioandikishwa ni 12,671 kati yao Wavulana ni 6,167 na
Wasichana ni 6,504 sawa na asilimia 84 ya wanafunzi 15,019 waliotarajiwa kuandikishwa
katika wanafunzi walioandikishwa 51 wameandikishwa kama wanafunzi wenye
mahitaji maalum  kati yao Wavulana 27 na
Wasichana 24”.

“Sambamba
na uandikishaji wa wanafunzi walio katika mfumo rasmi wa Elimu, pia wanafunzi
205 walio nje ya mfumo rasmi wa Elimu (MEMKWA) waliandikishwa kati yao Wavulana
119 na Wasichana 86”.
amesema Dkt. Yunge

“Halmashauri
ina jumla ya shule za sekondari 33 ambapo jumla ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga
na kidato cha kwanza kwa Mwaka 2024 ni 7,173 kati yao Wavulana ni 2,972 na
Wasichana 4,201 lakini wanafunzi walioripoti shuleni ni 6877 sawa na asilimia
96 kati yao Wavulana ni 2,839 sawa na asilimia 95 ya lengo ambapo Wasichana ni 4,038
sawa na asilimia 96 ya lengo la wanafunzi 7, 173 wanaotarajiwa kuripoti shuleni”.

“Halmashauri
katika kipindi cha Januari Mwaka huu 2024 imepokea Fedha za miradi ya maendeleo
kutoka Serikali kuu kiasi cha Shilingi 541, 800, 000.00 kwa ajili ya
miundombinu ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mgao ambao ni kwa mujibu wa
maelekezo kutoka Serikalini ambapo ni ukamilishaji wa maboma 2 ya vyumba vya
Madarasa , ujenzi wa matundu 56 ya vyoo pamoja na ujenzi wa vyumba 17 vya
Madarasa”.
amesema Dkt. Yunge

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nikodemus Luhende Simon akizungumza kwenye Baraza
la Madiwani Alhamis Machi 7,2024.

Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani Halmashauri
ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Nikodemus Luhende Simon akizungumza kwenye Baraza
la Madiwani Alhamis Machi 7,2024.

  

Diwani kata ya Ilola Mhe. Amosy Mshandete akizungumza kwenye Baraza la Madiwani leo.