Baraza la wafanyakazi la halmashauri ya wilaya ya meru lapitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022. baraza la wafanyakazi la halmashauri ya meru

 

Imewekwa: February 24th, 2021

Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Meru, Wilayani Arumeru limepitia rasimu ya bajeti ya Halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022 yenye jumla ya shilingi bilion 46.3.

Mwenyekiti wa Baraza hilo Ndg.Emmanuel Mkongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri, ametoa wito kwa  watumishi kuongeza juhudi na ufanisi katika utendaji wao kwani jukumu kubwa la Halmashauri ni kutoa huduma kwa wananchi.

Mkongo ametaja changamoto zinazo athiri utoaji wa huduma ilkiwemo ulipaji wa stahiki mbalimbali za watumishi kwa wakati, kufanya kazi kwa mazoea na uwezo mdogo  wa Halmashauri kujitegemea. Hivyo, ametoa wito kwa watumishi kuongeza juhudi, ufanisi  na ubunifu katika kuongeza uwezo wa Halmashauri kujitegemea “uwezo wa Halmashauri hii kujitegemea ni asilimia 7  hivyo hatuna budi kuongeza juhudi na uwajibikaji kwa kutoa huduma bora na kubuni vyanzo vipya vya mapato kuongeza  ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa vyanzo vilivyopo “amesisitiza Mkongo.

Mkongo amefafanua  bajeti hiyo yenye jumla ya shilingi bilioni 46.3 inahusisha mapato ya ndani jumla ya shilingi bilioni 3.4, ruzuku ya mishahara Shilingi bilioni 35.7, ruzuku ya matumimizi mengineyo ni shilingi bilioni 1.7 na ruzuku ya miradi ya maendeleo ni shilingi bilioni 5.2.

Wakichangia kwa nyakati tofauti, watumishi wameiomba Serikali kuongeza umri wa ukomo wa watoto katika bima ya afya ya Taifa (NHIF) kutoka miaka 18 hadi 23 kwani jambo hilo ni kikwazo kikubwa kwao “mtumishi unawajibika kumlipia mtoto wako huduma za afya ambaye ana umri wa miaka  chini ya 25 ambaye yupo Chuo Kikuu kwa kigezo cha umri kuzidi miaka 18” amesema Bi. Felister Lonjini

Aidha  watumishi hao wameiomba Serikali kuwawezesha watumishi wanaojiendeleza kitaaluma  kupanda madaraja na vyeo bila kuondoa miaka ambayo wameitumia masomoni sambamba na kuwajulisha watumishi sababu za kupanda au kutopanda vyeo.

Viongozi wa vyama vya wafanyakazi wameipongeza Halmashauri  kughulikia maslai ya watumishi wastaafu na kutoa wito kwa Halnashauri kuwajengea watumishi uelewa wa maswala yanayogusa stahiki zao ambapo  Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya TUGHE (M), ndugu Samweli Magero ameomba Halmashauri kutoa elimu  juu ya stahiki kwa Watumishi  wanaojiendeleza.

Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Halmashauri ya Meru Ndg.Emmanuel Mkongo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri,kushoto ni Katibu wa baraza hilo Bi.Oliver Swatty.

Wakuu wa idara wakati wa mkutano baraza la wafanyakazi.

Mkuu wa idara ya utawala na rasilimali watu Bi. Grace Mbilinyi akitoa  ufafanuzi wa maswala mbalimbali ya kiutumishi yaliohojiwa wakati wa baraza la wafanyakazi.

Katibu wa Chama cha wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya TUGHE (M), ndugu Samweli Magero akizungumza wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

Watumishi na viongozi wa watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.

Watumishi na viongozi wa watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.

Watumishi na viongozi wa watumishi wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.

Watumishi  wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.

Watumishi  wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.

Watumishi  wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.

Watumishi  wakati wa Mkutano wa baraza la wafanyakazi.

Bi. Angela Urasa ,Miongoni mwa watumishi waliotoa maoni