Basi lapinduka morogoro….9 wajeruhiwa

Watu
9 wamejeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la kampuni Kidinilo
kuacha njia jana  Alhamisi Januari 9, 2020 na kupinduka eneo la Mangae
barabara ya Morogoro Iringa huku chanzo kikitajwa ni uzembe na
mwendokasi.


Basi
lililokuwa kilitokea Ifakara kwenda Dar es Salaam lilikuwa na abiria
68  kwamba majeruhi watatu hali zao sio nzuri kutokana na majeraha
makubwa waliyoyapata na wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa
Morogoro

Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa, ameeleza chanzo cha
ajali hiyo ni Dereva wa Basi la Kidinilo kutaka kulipita gari jingine
bila kuchukua tahadhari, Dereva huyo anaitwa Shabani Sultan (54)
amekamatwa wakati akijaribu kutoroka kwa kutumia Bodaboda. 


“Kati
ya majeruhi tisa walionusurika kwenye ajali ya basi la Kidinilo, wawili
wamevunjika miguu, mmoja hali yake si nzuri, wengine wamepata majeraha
ya kawaida wanapatiwa matibabu” – RPC, Morogoro, Wilbroad Mutafungwa.