Breaking news, haya hapa matokeo ya darasa la saba 2019

Matokeo ya darasa la saba 2019,
yametangazwa. NECTA imeeleza ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.78.
Waliofaulu ni asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369. Pia Watahiniwa 909
wamefutiwa matokeo kwa sababu mbalimbali ikiwemo udanganyifu.



Katibu Mtendaji wa NECTA Dkt Charles Msonde
amesema
mwanafunzi aliyeongoza Kitaifa ni Grace Manga kutoka Shule ya Msingi
Graiyaki Mara, akifuatiwa na Francis Gwagi kutoka Shule ya Msingi
Paradise ya Geita.





Amesema kuwa aliyeshika nafasi ya tatu
ni Loi Kitundu kutoka Shule ya Msingi Mbezi ya Dar es Salaam, na
Victor Godfrey kutoka Graiyaki ameshika nafasi ya nne.

“Katika ufaulu wa masomo, somo la Kiswahili, Kiingereza na Sayansi
katika mtihani huo ufaulu wake umepanda na somo la Hisabati umeshuka,”