Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amewaongezea siku saba zaidi watuhumiwa wa uhujumu uchumi kuwasilisha barua zao kwa mwendesha mashtaka wa Serikali (DPP), endapo wanataka kufutiwa mashtka yao na kulipa fedha wanazodaiwa kwa makosa wanayotuhumiwa nayo.
Akizungumza wakati akipokea taarifa ya wahujumu uchumi waliokwisha kukiri makosa yao na kuonba kusamehewa ili walipe fedha wanazodaiwa, Rais Magufuli amesema amepoteka ombi la mwendesha mashtaka wa Serikali la kuongezewa siku tatu lakini anaongeza siku saba ili kutoa haki kwa wenye nia ya kusamehewa kuwasilisha barua zao.
Amesema waliokwisha wasilisha barua zao kuomba kuachiliwa ili walipe fedha wanazodaiwa ni zaidi ya watuhumiwa 400 na bado wapo ambao barua zao zimekwama katika magereza mbalimbali nchini kutokana na sababu tofauti tofauti.
Rais Magufuli amesema msamaha unaotolewa hautawahusu watuhumiwa wapya watakaokamatwa baada ya msahama huo na kumuagiza DPP kuwafikisha watuhumiwa wapya mahakamani bila kutoa msahama mwingine wa aina hiyo.