Juu na chini ni picha ya pamoja ya viongozi wa kamati ya siasa ya wilaya pamoja na viongozi wa chama hicho wa kata za Ngarenaro na Sakina baada ya kuwapokea madiwani hao wastaafu ndani ya chama hicho wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya Joseph Masawe picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Arusha kimewapokea madiwani wawili wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema walijiunga na chama hicho kuunga Juhudi za mh.Rais na Mwenyekiti wa chama hicho Dkt John Magufuli.
Akiongea Mara baada ya kuwapokea ndani ya chama hicho Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha mjini Joseph Masawe amesema kuwa hakuna bei ya kumunua binadamu bali bali kila moja anatumia demokrasia ya kuamua sehemu anayoona inafaa kuweza kutekeleza haki yake ya kikatiba ikiwemo kutumia mawazo yake na akili kujiunga na vyama vya kisiasa ikiwemo CCM .
Ameeleza kuwa chama hicho hakijawahi kufikiria kununua watu bali kimejipanga kuahughulika na shida za wananchi ndio maana wenye ufahamu wanaona ndio sehemu sahihi ya kufanyakazi za kuwatumikia wananchi kuwaletea maendeleo.
“Chama chetu hakijui bei ya kumunua mtu hivyo wanaojiunga na Cha hichi wanafuata mazuri ya ndani ya CCM ikiwemo kazi nzuri ya Mwenyekiti wetu taifa na Rais Dkt.John Magufuli sio vingine ni kuunga kuonyesha Juhudi za Rais katika kuwatumikia watanzania”
Kwa upande wake Katibu wa ccm wilaya chama Mwita Zakaria amesema kuwa chama hicho hadi Sasa teyari kimewapokea waliokuwa madiwani kwenye halmashauri ya jiji la Arusha 12 ikiwemo hao wawili
Ameeleza kuwa Cha hicho kimeanda utaratibu wa kuwapokea kwenye kata zao hapo baadae kwa kuwa sasa Kuna Ugonjwa wa Covid 19 au virusi vya Corona nao wanaheshimu maelekezo ya Serikali kutokuwa na mikusanyiko isiyo ya lazima ndio maana wakaamua kufanya mapokezi hayo na kamati ya siasa ya wilaya.
*Chama chetu kina wanachama lukuki hawa isingekuwa Ugonjwa wa Covid 19 ambao maelekezo ya Serikali yanatutaka tusifanye mikusanyiko isiyo ya lazima tungefanya mikutano kwenye kata zao kuwapokea kwa kuwa tunao wanachama lukuki ndani ya kata hizo”
Nae Isaya Doita alisema kuwa anashukuru kwa mapokezi hayo na kuahidi ushirikiano wa hali ya juu kuhakikisha chama hicho kinarudisha Jimbo la Arusha mikononi mwa CCM wakati ukifika
Alisema wanaodhani amenunuliwa wafute dhana hiyo kwani kwa mwenye akili haambiwi tazama anaona matukio yanayoendelea ndani ya chama katika kushughulikia shida za wananchi kama ilani CCM inavyoelekeza .
Awali akiongea Damuni Melimali alisema kuwa msingi wa chama hicho ni mkubwa ndio maana akaamua kujiunga na CCM kuunga mkono Juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya Dkt.John Magufuli kwa utumishi uliotukuka unaojali wanyonge ndio maana akaamua kwa dhati yake bila ushawishi kujinga kushirikiana nae kujenga taifa hili. |