Chama cha tughe mkoa wa shinyanga chawaomba watumishi wa umma kujiunga ili kunufaika na fursa zilizopo

Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa
serikali na Afya Tanzania (TUGHE)  Mkoa
wa Shinyanga Dkt. Allan Masanja amewaomba watumishi wa umma ambao hawajajiunga
na chama hicho waweze kujiunga ili kunufaika na fursa zilizopo.

Ameyasema hayo baada ya kushiriki kikao
cha pamoja cha viongozi wa kamati tendaji TUGHE Mkoa wa Shinyanga ambapo
amesema ni muhimu kila mtumishi mwenye sifa kujiunga na chama hicho na kwamba
pamoja na mambo mengine chama hicho kinasaidia kuzuia migogoro ya wanachama
katika sehemu zao za kazi.

Amesema zipo fursa mbalimbali wanachama wa
TUGHE wananufaika nazo ikiwemo elimu mbalimbali za namna ya utekelezaji wa
majukumu  sehemu za kazi katika kutimiza
wajibu wa mfanyakazi, namna ya kupata mafao baada ya kustaafu , namna ya
kujiandaa kustaafu pamoja na kutatua changamoto za wafanyakazi.

Dkt. Allan ambaye pia ni mjumbe wa kamati
ya utendaji ya Baraza kuu Taifa (KUBK) ametumia nafasi hiyo kuwaomba watumishi
wengine ambao bado wahajajiunga na chama cha TUGHE Mkoa wa Shinyanga, wajiunge
ili waweze kunufaika na fursa zilizopo ndani cha chama.

“Tunapokuwa
katika majukumu yetu ya chama kwanza tunawahamasisha wanachama wetu wajue
umuhimu wa chama kinavyoweza kuwasaidia katika shughuli zao za kiutumishi
wakiwa kazini, mahali pa kazi hata sehemu yoyote ile ambayo wao wanawajibika
kama watumishi wa umma”.

“Kazi
yetu ni kuhakikisha kwanza tunazuia migogoro ya wafanyakazi na mwajiri
inayoweza kujitokeza aidha wakati mwingine mtumishi anaweza kufanya kosa bila
kujua lakini chama kinaweza kumuelimisha majukumu yake na wajibu wake akiwa
sehemu za kazi pamoja na hayo sisi ni kiunganishi tunapeleka hoja zetu kwa
mwajiri ambazo watumishi wamezitoa sehemu za kazi kwa kutaka kuelewa stahiki na
changamoto ambazo wafanyakazi wanazipata”
amesema
Dkt. Allan

“Mfumo
wetu upo ndani ya matawi ambapo wanachama wanawasilisha changamoto zao ngazi ya
matawi nao wanasiwasilisha ngazi ya Wilaya badae zinawasilishwa ngazi ya Mkoa tukishajadili
ngazi ya Mkoa badae tunazituma ngazi ya Mkoa kwa ajili ya utatuzi”.

“Lakini
mara tu mtumishi anapoingia kwenye mgogoro cha cha TUGHE kinawanasheria ambapo
inapoonekana wanachama wetu ameingia kwenye kosa ambalo yeye hakutarajia au
hakukusudia kulifanya anajikuta aidha anapelekwa Mahakamani au anasimamishwa
kazi wanasherea wetu wa TUGHE wanamsaidia kutatua”.
amesema
Dkt. Allan

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati za wanawake
TUGHE Mkoa wa Shinyanga na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa ambaye pia ni afisa muuguzi
msaidizi katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Experantia Misalaba amesema
kupitia chama hicho wanawake wameendelea kuinuka kiuchumi kutokana na fursa
zilizopo ikiwemo miradi mbalimbali wanayoiendesha.

Amesema miradi hiyo inawasaidia wanawake
kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja ambapo naye
 amewaomba watumishi wa umma wanawake Mkoa wa
Shinyanga kujitokeza kwa wingi kwenye
 
chama cha TUGHE ili kuendeleza umoja katika kutatua changamoto za
wanawake.

Kikao cha pamoja cha viongozi wa kamati
tendaji TUGHE Mkoa wa Shinyanga kikiendelea katika ukumbi wa mikutano Liga
Hotel Manispaa ya Shinyanga.