Chama cha wafanyabiashara wanawake tanzania ‘twcc’ chatoa mafunzo kwa wajasiriamali kagera

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Chama Cha wafanyabiashara wanawake Tanzania
(TWCC ) Mwajuma Hamza wakati akitoa mafunzo kwa wajasiariamali wanawake
Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Na Ashura Jumapili, Bukoba
Chama cha Wafanyabiashara Wanawake Tanzania (TWCC) kimetoa mafunzo
kwa Wajasiriamali Wanawake mkoani Kagera kuhusu namna ya kutumia fursa
za kibiashara maeneo ya mipakani sanjari na kujua sheria,kanuni na
taratibu za kuvuka mipaka ambapo jumla ya wanawake 100 watakaonufaika na
mafunzo hayo ya siku nne.
Kaimu Mkurugezi Mtedaji wa Chama hicho Mwajuma Hamza,alisema lengo la
chama hicho ni kuwaunganisha Wanawake wote Wajasiriamali wa Tanzania ili
wawe na umoja ,nguvu ,sauti na mikakati ya pamoja katika biashara
hivyo wanawafundisha wanawake namna ya kufanya biashara za mipakani
,kutumia fursa za biashara za Jumuia ya Afrika Mashariki,kanuni,taratibu
na sharia za kufanya biashara maeneo ya mipaka.

Alisema soko la Afrika Mashariki ni kubwa na Tanzania inazalisha vitu
vingi ambavyo nchi jirani hawazalishi hivyo hiyo pia ni fursa moja wapo
kwa wajasiramali hao.

“Tunataka Wanawake waingie kwenye uchumi wa viwanda na waweze kuzalisha
Zaidi bidhaa zenye tija na ubora unaokubalika na soko la
kimataifa”,alisema Hamza.
Alisema chama hicho kilianza mwaka 2005 kimesajiliwa kwa mujibu wa
sharia na kina Zaidi ya wanachama ( 5000 )nchi nzima pia kina ofisi
mikoa 10 na mwezi Machi mwaka huu wanatarajia kufungua ofisi nyingine
Mkoani Kagera.
 Alisema pia wanawasaidia wajasiriamali
wanawake kupata taarifa za masoko ,kuzalisha bidhaa zenye ubora
zinazokidhi soko la ndani n nje ya nchi, kuongeza uzalishaji na jinsi ya
kuweza kupata mitaji ya kuendesha biashara zao.

Alisema wamezindua mfumo wa kuripoti vikwazo vya kibiashara maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya mipaka.

Mgeni rasmi katika mafunzo hayo,Afisa biashara mkoa wa Kagera
,akimuawakilisha katibu tawala mkoani humo Prof.Faustine Kamuzora,
alisema Tanzania ina fursa nyingi zinazotokea duniani ambapo inapakana
na nchi nane.
Tendega,alisema mkoa wa Kagera unapakana na nchi nne ,Jumuia ya Afrika
Mashariki ina watu wasiopungua milioni 190 ni ukanda wa watu wengi na
kudai kuwa Watu hao ni soko kwa bidhaa zinazozalishwa Tanzania.
Alisema Kanda ya ziwa inachukua asilimia 14 ya watu wote wa nchi hii pia ni fursa ya kuweza kupeleka bidhaa huko.
Alisema hali ya hewa ya mkoa wa Kagera ni nzuri ina misimu miwili ya
mvua na pia kuna ziwa Victoria linafaa kwa shughuli mbalimbali za kilimo
na uvuvi.
Alisema mkoa unakabiliwa na changamoto moja ya uzalishaji mdogo wenye viwango hafifu .
Alisema ili kukabiliana na uzalishaji mdogo ni vyema wajasiriamali
wakaungana na kushirikiana kuongeza tija katika uzalishaji wa bidhaa
mbalimbali.
“Chuki kwenye biashara ni mwiko,mshirikiane kuunganisha mawazo,nguvu na
mitaji ili kuwa na mshikamano katika biashara zenye ubora na
tija”,alisema Tendega.
Alisema Mkoa umefanya jitihada mbalimbali za kumkomboa mwanamke ikiwemo
kuanzisha madawati mbalimbali ya mkoa na wilaya lengo likiwa kuwawezesha
wanawake kiuchumi na kuwaweka pamoja kuchangamkia fursa mbalimbali.
Kaimu meneja wa shirika la kuhudumia viwanda vidogo vidogo (SIDO )Mkoani
Kagera Peter Kilima,alisema wajasiriamali hao watapata fursa ya
kujifunza na kuelewa pamoja na kukabiliana na changamoto za kibiashara
wanazokutana nazo.
Kilima,alisema SIDO wamejipanga kuwasidia wajasiriamali katika kuwapatia
mitaji kwa kutwapatia mikopo ya kiasi cha shilingi laki 5 hadi milioni
moja.
Akiongea kwa niaba ya Wajasiriamali wenzake Jovita Banyeza ,alisema
mafunzo hayo yatawasidia kutambua na kuibua fursa za kibiashara zilizopo
mipakani.
Banyenza,alisema ndio mwanzo wa kuzifungua na kuwajibika katika fursa hizo za kibiashara kwa wanawake .
Alisema mikopo isiyokuwa na riba kwa wanawake inayotolewa na halmashauri
imekuwa chachu kwa wafanyabiashara wanawake ambao sasa wameamka na
kujikita katika biashra mbalimbali.