Daktari matatani kwa kuwafunga vizazi wanawake 126 bila ridhaa yao

Daktari mmoja anatuhumiwa kwa kufanya upasuaji kwa wanawake na kutoa
viungo bila ridhaa zao, mmoja wa wagonjwa wake amemtuhumu na kumfikisha
mahakamani.
Amefikishwa katika mahakama huko Virginia nchini Marekani.
Dr Javaid Perwaiz dakatari bingwa wa kina mama, amewadanganya wanawake
kuhusu afya zao na kuwasababishia majeraha makubwa, kwa mjibu wa shirika
la upepelezi la marekani FBI.
Tangu kukamatwa kwake tarehe 8 novemba , zaidi ya wanawake 126 wameripoti na kulalamika kuhusu tabia zake.
Siku ya alhamisi , jaji wa mahakama alitoa amri ya kukamatwa kwa Dr Perwaiz wakati akisibiri hukumu yake.
Kwa mujibu wa hati ya kukamatwa ya FBI Dr.Perwaiz anatuhumiwa kutoa
majibu ya uongo ya kiafya na kufanya upasuaji usio wa lazima kwa
wagonjwa wake na bila ridhaa zao.
Amefanya upasuaji wa kutoa sehemu za uzazi za wanawake bila ridhaa zao
pamoja na kufunga uzazi. Daktari huyo ana ofisi mbili eneo la
Chesapeake, jimbo la Virginia nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa mahakamani, katika kipindi cha
mwaka 2014-18 Dr Perwaiz amefanya upasuaji kwa asilimia 40 ya wanawake
wanaopokea matibabu wakiwa na kipato cha chini.
Katika kundi la wagonjwa wanawake 510,asilimia 42 walifanyiwa angalau upasuaji wa aina mbili.
Shirika la upepelezi la FBI lilipewa taarifa kwa mara ya kwanza mwaka 2018 na muuguzi ambae alisikia kutoka kwa mgonjwa mmoja.
”Wagonjwa wanasema kuwa walikua wakisikia Dr Perwaiz akitaja sana
kuhusu saratani na kuwatisha waweze kufanyiwa upasuaji” anasema Afisa
wa FBI Desiree Maxwell.Daktari huyu amekua akiwafunga vizazi wanawake bila ridhaa zao.
Wakili wa Dr Perwaiz hakujibu baada ya kutafutwa na BBC siku ya Alhamisi.
Dr Perwaiz amesoma masomo yake ya utabibu huko Pakistani na alipata leseni ya kufanya kazi Virginia Marekani mwaka 1980.
Mwaka 1982 alipoteza sifa zake za kufanya kazi katika hospitali huko Maryland kutokana na maamuzi mabaya ya kitabibu.
Kwa mujibu wa FBI alifanyiwa uchunguzi mara ya kwanza na bodi ya
madaktari wa Virginia kwa kufanya upasuaji bila kuwa na maamuzi yasiyo
na weledi wa kitaaluma.
Baada ya kukubali hatia ya kukwepa kodi 1996, alinyang’anywa leseni kwa miaka miwili.
Chanzo – BBC