Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Moshi Lyobaa akitaja huduma za Afya zinazopatikana katika Hospitali hiyo huku akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma bora.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Moshi Lyobaa amewaomba wakazi wa Mkoa wa Shinyanga kujitokeza kwa wingi kupata huduma mbalimbali za magonjwa ya nje na magonjwa ya ndani katika Hostitali hiyo.
Ametoa wito huo wakati akizungumza na Misalaba Media ambapo amesema kwa sasa Hospitali hiyo inatoa huduma zote kwa wananchi ikiwemo huduma ya meno, huduma ya matibabu kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, Huduma za matibabu kwa wajawazito na watoto wachanga pamoja na huduma za matibabu ya dharura.
Amewaomba wananchi kujitokeza ili kupata huduma kwa uharaka huku akiishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya uboreshaji wa majengo pamoja na vifaa vya kutolea huduma katika Hospitali hiyo ya Manispaa ya Shinyanga.
“Katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga huduma zipo na zinaendelea kuna huduma za magonjwa ya nje, kuna huduma za magonjwa ya ndani, kuna huduma za matibabu kwa wajawazito na watoto wachanga, kuna huduma za upasuaji kwa wa mama wajawazito, kuna huduma za Mionzi tunavifaa vya kisasa kwa kweli tunamshukuru sana Rais Samia kwa sababu ametuwezesha kupata vifaa vya kisasa ambavyo vinatuwezesha na kuturahisishia kazi zetu”.
“Lakini pia tunahuduma ya Meno kuna mashine ya kisasa ya kung’olea Meno ambayo tumeipata hivi karibuni tunaomba sana wagonjwa watu wote wenye changamoto waje kupata huduma kwa sababu mashine ipo na niya kisasa zaidi huduma zingine tunazozitoa ni huduma ya Macho, huduma za matibabu ya dharura yaani kwa wale ambao wanahitaji huduma ya dharura kwa ukaribu naya haraka kuna madaktari wakutosha na manesi wakutosha wenye uzoefu kwahiyo hizo huduma zote zinapatikana hapa kwenye Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga”.
amesema Daktari Moshi
“Pia tunahuduma za Maabara tunapima na tunamashine za kisasa zote zinafanya uchunguzi wa magonjwa yote tunahuduma pia ya matibabu kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI pia tunahuduma ya baba mama na mtoto yaani tunahudumia kwa kupima wajawazito, kupima watoto wadogo chini ya Miaka mitano pamoja na chanjo”.
“Tuna Magari mawili ya Ambulance ambayo hata kama kuna changamoto wagonjwa tunaweza kuwasafirisha haraka kuwapeleka katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa na ni bure labda niseme kwamba kwa taratibu za huduma za Afya huduma huwa zinapatikana masaa 24 siku saba (Jumatatu hadi Jumapili) kwa maana ya kwanza Hospitali huwa haifungwi muda wote tunatoa huduma masaa yote 24 changamoto ilikuwa ni kwamba watu walikuwa wakipita wakiona ukarabati wanaona kwamba hii Hospitali haipo lakini niseme kwamba Hospitali ipo na huduma zote zinapatikana hapa japo kuwa mnaona tunaendelea na ukarabati lakini ni kuboresha tu maeneo ya kufanyia kazi lakini huduma zote zipo zinaendelea kwahiyo watu wote karibuni sana kupata huduma na ukizingatia hapa ni mjini katikati”.amesema Daktari Moshi
Mratibu wa huduma za kinywa na Meno katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Anna Mwakapila amesema huduma ya kinywa na meno kwa sasa inapatikana muda wote baada ya kupokea vifaa vya kisasa kutoka serikalini.
“Huduma zetu niza kisasa kwanza tumepata kiti kizuri chenye asesor zote unaweza ukaziba Jino kwa dawa ya muda mfupi, unaweza ukaziba Jino kwa dawa ya muda mrefu, unaweza ukatibu mzizi wa jino, unaweza ukaondoa kiini cha Jino lakini pia kung’oa Jino lililoharibika vibaya hii ni hatua ya mwisho kabisa wananchi tunawakaribisha mjitokeze kwa wingi kupata huduma hii wataalam wapo ni wa kisasa wenye uzoefu, tunamshukuru Rais mama yetu Samia Suluhu Hassan kwa kuweze kufanikisha hii huduma”.amesema Mwakapila
Kwa upande wake mtaalam wa Mionzi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel ameeleza upatikanaji wa huduma za Mionzi katika Hospitali hiyo huku akiwaomba wananchi kujitokeza.
“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea mashine mpya na ya kisasa mashini hii ni ULTRASAOUND tunapima kwa lika zote wamama wajawazito, watoto, mabinti, vijana, wababa na wazee wote tunawahudumia kupitia hii mashine kwa wajawazito tunaangalia sana watoto ambao wapo tumbuni kama kuna changamoto yoyote mtoto amekaa ibaya au kuna shida yoyote hii mashine inatambua pia kwa wanaume sana sana wazee tunaangalia mambo yao ya uzazi sana sana changamoto za tezidume hii mashine inatambua kwahiyo tunawakaribisha sana wakazi wa Mkoa wa Shinyanga na maeneo jirani kuja kupata huduma hii”. amesema Evelyne
Daktari mfawidhi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Moshi Lyobaa akitaja huduma za Afya zinazopatikana katika Hospitali hiyo huku akiwaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupata huduma bora.
Mratibu elimu ya Afya kwa umma Manispaa ya Shinyanga Salmon Mkanula akionyesha vifaa vya kisasa katika chumba cha kutolea huduma ya kinywa na Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Mratibu elimu ya Afya kwa umma Manispaa ya Shinyanga Salmon Mkanula akiwakaribisha wakazi wa Shinyanga wanaosumbuliwa na Meno kwenda kupata huduma bora kwenye Hospitali hiyo ya Manispaa ya Shinyanga
Mratibu wa huduma za kinywa na Meno katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Anna Mwakapila akionesha vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya Meno katika Hospitali hiyo.
Mtaalam wa Mionzi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel akionyesha mashine ya ULTRASAOUND.
Mtaalam wa Mionzi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel akionyesha mashine ya ya kisasa ya X RAY.
Mtaalam wa Mionzi katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Evelyne Emmanuel akionyesha mashine ya ya kisasa ya X RAY.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
Vifaa vya kisasa katika chumba cha kutulea huduma ya Meno Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga.
TAZAMA VIDEO