Mmiliki mabasi ya sahara akutwa amekufa gesti

Mfanyabiashara
na mmiliki wa mabasi ya Sahara, Abdalah Msangi (47) mkazi wa Usangi
Mkoani Kilimanjaro, leo Jumapili Januari 5, 2020 amekutwa amekufa kwenye
moja ya nyumba ya wageni iliyopo Mtaa Dar es Salaam Mjini Moshi.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Kilimanjaro, Tanzania, James Manyama amethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Amesema mfanyabiashara huyo alikuwa na rafiki yake wa kike chumbani,
lakini baada ya kuona mwenzake anaishiwa nguvu na kuanza kutokwa na povu
puani na mdomoni akakimbia.
“Huyu Mfanyabiashara alikuwa na rafiki yake wa kike kwenye chumba cha
wageni huko Dar es Salaam street, baada ya kuona ameishiwa nguvu na
kuanza kutokwa na povu mdomoni alitoroka, amedai Kamanda Manyama.
Aidha, amesema baada ya kupata taarifa na kufika eneo la tukio na
kulipekua gari la Msangi kulikutwa dawa ya kienyeji ambayo imechukuliwa
kwa uchunguzi.
Amesema Mwili wa marehemu umepelekwa Hospitali ya Mkoa Mawenzi kwa uchunguzi zaidi.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *