Dc korogwe awahimza madereva bodaboda kujiunga na mpango wa bima ya afya

 MKUU
wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa akizungumza na madereva wa waendesha
pikipiki za magurudumu mawili na matatu wilayani humo kuhusu umuhimu wa
kujiunga na mpango wa bima ya afya wakati wa uzinduzi wa mpango huo kwao kushoto ni
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally
Mwakababu na kulia ni Mkuu wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu kulia akizungumza wakati wa uzinduzi huo


Mkuu wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola akizungumza wakati wa uzinduzi huo


AFISA Matekelezo wa NHIF Mkoa wa Tanga Macrina Clemence akisisitiza jambo


Mwenyekiti
wa Waendesha pikipiki za magudumu mawili na matatu wilayani Korogwe
Mohamed Kombo Kapaya akitoa ushuhuda kwa wenzake namna bima ya afya
ilivyomsaidia


Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
kulia akitoa elimu kwa mwendesha pikipiki za magurudumu matatu kabla ya
kuanza ufunguzi wa mpango wa elimu ya bima ya afya kwao katikati ni
Mkuu wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola


Meneja
wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu
kulia akitoa elimu kwa mwendesha pikipiki za magurudumu matatu kabla ya
kuanza ufunguzi wa mpango wa elimu ya bima ya afya kwao kushoto ni Mkuu
wa Usalama Barabarani wilaya ya Korogwe (DTO) Leonard Bandola

WAENDESHA Pikipiki za
magurudumu mawili na matatu wilayani Korogwe mkoani Tanga wamehimizwa
kuchangamkia fursa ya kujiunga na mpango wa bima ya afya ili waweze kuwa na
uhakika wa matibabu wanapokuwa wakiugua.

Hayo yalisemwa na
Mkuu wa wilaya ya Korogwe Kissa Gwakisa wakati akizindua mpango wa Bima kwa madereva
wa pikipiki za magurudumu mawili na matatu wilayani Korogwe uliofanyika kwenye
uwanja wa Mazoezi.

Alisema bima ya afya
ndio silaha pekee ambavyo inaweza kuwahakikishia uhakika wa matibabu wakati
wanapoumwa huku wakiwa hawana fedha hivyo ni muhimu kuichangamkia na kujiunga
nayo .

“Ndugu zangu maradhi
huja bila kutegemea hivyo niwasihi mhakikishe mnachangamkia fursa hii ya
kujiunga na mpango wa bima kwani ni mkombozi mkubwa sana na utakuwa na uhakika
wa matibabu “Alisema

Aidha alisema lakini
gharama za matibabu zimekuwa zikipanda kila siku hivyo iwapo watajiunga na
mpango huo wa bima utawasaidia kuwapunguzia gharama za kupata matibabu.

Awali akizungumza
wakati wa uzinduzi huo,Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga
(NHIF) Ally Mwakababu alisema lengo la kukutana na makundi hayo ni kuweza
kuwahamasisha wajiunga na mpango wa bima ya afya ambao ni muhimu kwa maisha yao
na unawahakikishia uhakika wa matibabu.

Alisema makundi hayo
ni moja ya watu ambao wanakabiliwa na changamoto za ajali wanapokuwa kwenye
shughuli zao hivyo kujiunga na mpango wa bima atawawezesha kupata huduma za
matibabu pindi watakapoungua.

Alisema kwamba
wanaweza kulipa kwa awamu kwa utaratibu wa kupitia kwa uongozi wao unaweza
kuzipeleka kwenye kupitia benki ya NMB ili wawezesha kunufaika na huduma za
matibabu badala ya kufikiria kupata fedha tunakwenda kufanyia mambo mengine.

“Ndugu zangu hakuna
anayejua ugonjwa utaingia muda gani au siku gani hivyo ni muhimu kuhakikisha
tunajiunga na bima ya afya kwa lengo la kuwa na uhakika wa matibabu pindi na
hii itawasaidia kuepuka kutumia gharama kubwa za matibabu”Alisema Mwakababu.

Naye kwa upande wake
Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki za magurudumu mawili na matatu wilayani
Korogwe mkoani Tanga
Mohamed Kombo Kapaya aliwashukuru mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga
(NHIF) kwa kuwakumbuka wao madereva wa kuwaingia kwenye mfumo wa matibabu kwa
gharama nafuu.

Alisema kwamba umuhimu
wa kuwa na bima ya afya ni mkubwa huku akitolea historia yake mwenyewe wakati
alipopata tatizo la kuugua mwaka 2011-2012 tukio ambalo lilisababisha kutoka kuhamishwa
kwenye Hospitali ya wilaya ya Korogwe na kuhamishiwa KCMC.

Mwenyekiti huyo
alisema wakati huo alikuwa akifikiria angewezeje kulipa gharama za matibabu
lakini kwa kuwa mke wake ni mwalimu alimkatia bima na hivyo kumsaidia katika
matibabu yake ambapo alifanyiwa upasuaji KCMC na huduma nyengine muhimu.

“Hivyo nieleza kwamba
kuna umuhimu mkubwa sana kuwa na bima ya afya naomba leo hii kila mtu ajiandikisha
na kujiunga kwenye mpango huu “Alisema