Dc mjema amjibu rc paul makonda

Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema pamoja na afisa utamaduni wa Wilaya
Cloude Mpelembwa wameeleza kuwa hawajakataza watu wasifanye ibada
katikati ya wiki.

Hayo
yamesemwa  na mkuu wa wilaya hiyo, baada ya mkuu wa Mkoa  wa Dar Paul
Makonda kutengua kauli ya awali ya mkuu wa wilaya ya Ilala ya kuwataka
wananchi kuto fanya ibada katikati ya wiki.

Mjema amesema kwamba watu wamemtafasiri vibaya kuwa amekataza  ibada ila amepinga wale wanao anzisha makanisa yasiyo rasmi.

“Wale
ambao wamejenga tu turubai na wameweka maspika hao lazima watuambia
wamesha sajiliwa na nimemuagiza afisa utamaduni aende akawaangalie kama
wamesajiliwa,” amesema  Mjema.

“Nataka
niliweke sawa kabisa mimi ni muumini mzuri wa kumuamini Mungu siwezi
kuzuia watu wasiende kuabudu tumesema kuna watu wanaanzisha makanisa
yasiyo stahili na ukiingia ndani ya makanisa hayo unakuta watu wa tano
au sita wanao sali jumatatu hadi jumatatu. Kazi wanafanya lini,” amesema
Mjema.

Naye
afisa utamaduni wa manispaa  hiyo  Mpelembwa, amesema  mkuu wa wilaya
hakuwa na kosa lolote bali alitoa ushauri kuwa matumizi ya vyombo vya
mziki visiwe kero kwa wananchi wengine na waumini wanatakiwa wafanye
kazi za kujiletea kipato.

“Siku
za ibada za msingi kabisa ni Ijumaa, Jumamosi na Jumapili, lakini
Jumatatu mpaka Ijumaa watu wanaruhusiwa kufanya ibada katika maeneo ya
ibada na ushauri ulitolewa kwamba wazingatie katika matumizi ya vyombo
vya muziki,” amesema Mpelembwa.