Na JOHN MUSYOKI, KIAMBERE MJINI
DEMU mmoja mjini hapa, alishangaza wapangaji alipoanza kulia akimlaumu mdosi wake kwa kutombusu.
Kitendo hicho kiliwafanya wafanyakazi wenzake kubaini kwamba demu huyo alikuwa na uhusiano wa mapenzi na mdosi ambaye ana mke na watoto.
Yasemekana uhusiano huo ulikuwa umeanza kuingia baridi na demu akamwendea mdosi na kumtaka ambusu.
“Kwa siku nyingi umenipuuza, hata salamu hakuna. Umenipiga chenga kwa muda mrefu sana licha ya kuwa ninakupenda. Unaumiza moyo wangu sana na sasa ninataka busu,” demu alimwambia mdosi wake.
“Pole sana hata kama ninakupenda sitaki kuendelea kuzozana na mke wangu. Niwie radhi kwa sababu siwezi kukupa busu kwa sasa, endelea na kazi,” jamaa alisema.
Kulingana na mdokezi, buda alimpuuza demu na kutoka nje lakini demu alimfuata huku akipiga kelele na kulia.
“Demu alizidi kulia mpaka wenzake wakaenda kujua kilichokuwa kikijiri na kufahamu kuwa demu alikuwa analilia busu kutoka kwa mdosi wake,” alieleza mdokezi.
Hata hivyo, haikujulikana kilichojiri baada ya kioja hicho. Pia aikujulikana ikiwa mkewe bosi alipata habari kuhusu tukio hilo la kustaajabisha.