Dr. bashiru: rais magufuli arejesha matumaini mapya kwa wanyonge

Katibu
Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally ameweka wazi kuwa,
jambo moja kubwa lililofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini Mhe.
Rais John Pombe Magufuli ni kurejesha matumaini mapya kwa wanyonge na
wavuja jasho waliokuwa wamekata tamaa.


Amesema
kuwa, wanaCCM wote, watembee kifua mbele kwani, kati ya mambo makubwa
ambayo serikali ya CCM ya awamu ya tano imeyafanya ni kurejesha
matumaini ya wanyonge, ambapo hilo pekee ni jambo kubwa na limeleta
faraja kwa watu wengi, sasa wanaimani kubwa na CCM.

Ameyasema hayo jana tarehe 19 Januari, 2020 Kigoma Mjini akizungumza na viongozi wa Mashina, Matawi, Kata, Wilaya na Mkoa.

“WanaCCM
tembeeni kifua mbele, kati ya mambo ambayo awamu ya tano imeyafanya na
makubwa hayatasahaulika, ni kurejesha matumaini ya wanyonge, na hilo
katika siasa ni jambo kubwa, matumaini mapya kwa watu waliowahi kukata
tamaa, matumaini mapya kwa wavuja jasho, matumaini hayo yamerejea chini
ya uongozi shupavu, uongozi wenye maono, uongozi wa kizalendo wa Dkt.
John Pombe Magufuli.”

Ameongeza
kuwa, “wanaCCM mkiulizwa ni jambo gani jipya limefanyika linalopimika ,
linaloonekana kila mahala na kila mwenye akili na nia njema, waelezeni
bila kupepesa macho, jambo kubwa jipya ni kurejesha matumaini mapya kwa
wanyonge.”

Amesisitiza
zaidi kuwa, kila analolifanya Mhe. Rais Magufuli, kila analolisimamia
na kila analoliamua ni kwa maslahi ya kuwapa matumaini mapya watanzania
wavuja jasho na katika hili mpaka sasa ameacha alama kubwa, ukiacha
ujenzi wa barabara, reli, madaraja na mengine mengi anayoyafanya.

Aidha,
Katibu Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wanaCCM wote kuwa, Chama
Kimejipanga vya kutosha kurejesha Jimbo na Halmashauri ya Kigoma Mjini
ambapo kwa sasa vyote vinaongozwa na upinzani, hivyo wanachama wote
waendelee kuwa na umoja na mshikamano zaidi.

Wakati
huo huo, Katibu Katibu amegawa vitambulisho kwa wenyeviti wa mashina
ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo kwa wenyeviti hao nchi nzima
kupatiwa vitambulisho na watambuliko katika ofisi zote za Umma.

Mkutano
huo wa ndani umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali
wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Ndg. Amandus Nzamba na
Mkuu wa Mkoa huo Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga.

Leo
Katibu Mkuu amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu Mkoani
Kigoma iliyolenga kuimarisha na kuhuisha uhai wa Chama, ambapo tayari
amewasili Dar es Salaam kuendelea na Majukumu ya kikazi.