Ewura yafanikiwa kudhibiti uchakachuaji mafuta

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
hiyo  Zinyangwa Mchani,akizunguzma  wakati wa semina ya waandishi wa
habari waliopo Mkoa wa Dodoma
Sehemu ya waandishi wa habari wakifatilia  semina  iliyoitishwa na EWURA kutoa Elimu juu ya Sekta hiyo.
Na.Alex Sonna,Dodma
Mamlaka ya Udhibiti ya Nishati na Maji,Energy and Water Utilities
Regulatory Authority[EWURA] imefanikiwa kudhibiti Uchakachuaji
wa Mafuta kutoka asilimia 74% kwa mwaka 2007 na hadi kufikia asilima 4%
pekee kwa mwaka huu 2019.
Hayo yalisemwa  Novemba 1,2019 na
Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka hiyo,Bw.Zinyangwa Mchani wakati akitoa
wasilisho la Mamlaka hiyo kwenye semina na waandishi wa Habari jijini
Dodoma.
Bw.Mchani ambaye pia ni mkurugenzi
wa Uchumi EWURA amesema hiyo ni kutokana na sera nzuri ya Mamlaka hiyo
ilivyojipanga kwa sasa pamoja na utendaji maridadi wa wafanyakazi wake
na kuongeza kuwa uchakachuaji wa Mafuta ilikuwa changamoto kubwa hapa
nchini.
Aidha,Bw.Mchani amesema EWURA
imeokoa jumla ya Tsh.Bilioni 121.6 kwa mwaka 2012 na 2013 hali imetokana
na kuandaa na mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja.
Katika hatua nyingine Bw.Mchani
amesema ,ili kukabiliana na Upungufu wa Mafuta hususan maeneo ya
Vijijini EWURA imeanzisha kuruhusu mfumo wa Vituo vya mafuta vinavyo
vinavyotembea .
Ameendelea kufafanua kuwa,EWURA
imefanikiwa kutoa Leseni 1561 za biashara ya Mafuta ,ambapo leseni za
biashara za jumla ni 66 na rejareja ni 1397.
Kuhusu suala la Maji ,Kaimu
Mkurugenzi huyo wa EWURA amesema mamlaka hiyo imekuwa na changamoto ya
kudhibiti mamlaka za maji 130 kati ya hizo 95 ni za Wilaya hivyo inakuwa
changamoto kubwa katika uendeshaji

wake.
 
Hata hivyo,EWURA Mnamo Tarehe 8,Juni,2015 ilishinda tuzo ya ya Energy ya Regulator of the Year Award.
Ikumbukwe kuwa EWURA ilianzishwa
kwa Mujibu wa Ibara ya 4 ya Sura ya 414 ya sheria ya Tanzania na ilianza
kufanya kazi Septemba ,2006 kwa dhumuni la kudhibiti huduma za
nishati,[Umeme,Petrol, na Gesi asilia]na Maji na Usafiri huku ikiwa na
Majukumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kusimamia masuala ya leseni