Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi
akizungumza katika halfa ya kukabidhi magari 9 kwa taasisi za TAWIRI,
Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Bodi ya Utalii (TTB) ,Tume ya Taifa ya
Umwagiliaji (NIRC) ,Bonde la Mto Rufiji (RBWB) ,na Timu ya Uratibu
kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuimarisha utendaji
kazi wa taasisi hizo katika shughuli za mradi wa REGROW. Makabidhiano
hayo yalifanyika jijini Dodoma.
Mratibu
wa Mradi , Aenea Saanya akizungumza kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu
kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya Mradi wa Regrow iliyofanyika
jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi akikata
utepe katika hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW huku
akishuhudiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki, Dkt. Ezekiel
Mwakalukwa na mwakilishi wa Tawiri, Dkt. Wilfred Mareale.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi
akimkabidhi funguo za gari mwakilishi wa TAWIRI, Dkt. Wilfred Mareale
kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa REGROW jijini
Dodoma.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ( katikati) akiwa
kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa Taasisi baada ya kukabidhiwa
funguo za magari kwenye hafla ya makabidhiano ya magari ya mradi wa
REGROW jijini Dodoma.
(Picha zote na Gladys Lukindo- Afisa Habari, Wizara ya Maliasili na Utalii)