Benki ya kcb yasafirisha wafanyabiashara kwenda china

Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja wa wafanya biashara wa vipodozi Irene Moshi, wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye .


Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja
Masika Mukule akikabidhi tiketi kwa mmoja wa wafanya biashara wa
Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba, wakati wa kuwakabidhi
tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china kukutana na
wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na walanguzi
wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo makao
makuu ya KCB Dar es Salaam. (katikati), Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye .
Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye (kulia)
akizungumza wakati wa kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao
wanakwenda nchi china kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili
kuepuka kusumbuliwa na walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi
hafla hiyo imefanyika leo makao makuu ya KCB Dar es Salaam Wengine
pichani (watatu kushoto), Mkuu wa Kitengo cha wateja wadago na kati
Abdul Juma, Mkuu wa kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule pamoja na
Mfanya biashara wa Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba.
Mkuu wa Kitengo cha wateja wadago
na wakati Masika Mukule (watatu kushoto), akizungumza wakati wa
kuwakabidhi tiketi wateja wa benki hiyo ambao wanakwenda nchi china
kukutana na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali ili kuepuka kusumbuliwa na
walanguzi wakati wanapokwenda kufanya manunuzi hafla hiyo imefanyika leo
makao makuu ya KCB Dar es Salaam (kulia) Mkuu wa Kitengo Cha Masoko na
Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya KCB, Christine Manyenye, Mkuu wa
kitengo wa wateja rejareja Masika Mukule pamoja na Mfanya biashara wa
Kampuni ya Sadio Tours na Travel Saada Sipemba.
……………….
Benki ya KCB Tanzania kupitia KCB
Biashara Club yapeleka wafanyabiashara 10 kwenda nchini China kwa lengo
la kukutana na wazalishaji halisi wa bidhaa mbalimbali ili kujifunza na
kutafuta namna bora ya kuweza kuboresha biashara zao. Wafanyabiashara
hao watakaa nchini China kwa siku 10 na kupata fursa ya kutembelea miji
miwili mikubwa. 

Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam jana Mkuu wa Kitengo cha Masoko, Mahusiano na
Mawasiliano wa benki ya KCB, Christina Manyenye alisema wameanza
kuwapeleka China wafanyabiashara hao ambao ni wateja wa benki hiyo ili
wakakutane na wazalishaji halisi na si walanguzi au madalali ambao
uwauzia bidhaa kwa bei ya juu. 

Alisema kwa muda mrefu wafanyabiashara
nchini ambao wanakwenda China wamekuwa wakikumbana na changamoto
mbalimbali ikiwamo za lugha na kuuziwa vitu bei za juu hivyo kupitia
safari hizo wanazoziandaa mambo hayo hayatajitokeza. 

“Tatizo kubwa ambalo
wafanyabiashara walikuwa wanakutana nalo ni kuuziwa vitu kwa bei ya juu
na walanguzi au madalali sasa kupitia safari hii tutawakutanisha na wale
wazalishaji halisi ambao wanaviwanda ambapo watapata fursa ya
kutembelea viwanda vyao kisha kutoa oda za kutengenezewa bidhaa zao. 

Lakini pia kuna tatizo la lugha
kule, kupitia safari hii tuliyoiratibu sisi KCB Benki tutawapatia
wakalimani ambao watatembea nao kila mahali ili kurahisisha mawasiliano
yao na wazalishaji hao,” alisema. 

Naye Meneja Uhusiano wa Wateja
Wadogo na wa Kati wa benki hiyo, Moses Kisaka alisema wanamatumaini
kwamba siku hizo 10 wafanyabiashara hao wataweza kuzunguka na kukutana
na wazalishaji pamoja na kutumia fursa hizo kufanya manunuzi ya bidhaa
zao. 

Alisema wafanyabishara hao watakutana na wazalishaji halisi
watakaowauzia vitu kwa bei ya chini kuliko ilivyokuwa awali walipokuwa
wakienda wenyewe na kukutana na walanguzi waliokuwa wanawauzia vitu kwa
bei ya juu. 

“Tunafanya hivi kwa lengo la
kuwasaidia wapunguze gharama za kupata bidhaa, tunaamini safari hizi
zitakuwa ni muendelezo na tunatumaini mwakani kuwapeleka wafanyabiashara
wengi zaidi,” alisema. Aidha alisema benki hiyo imeanzisha kitengo cha
KCB Biashara Club kwa lengo la kuwakutanisha pamoja wafanyabiashara
mbalimbali na kuzungumza juu ya changamoto na fursa za kibiashara
wanazokutana nazo. 

Kwa upande wake Mwakilishi wa
wafanyabiashara wanaoenda China, Saada Sipemba alisema safari hiyo
itawasaidia kupata fursa ya kuona maonyesho makubwa yanayofanywa na
wenye viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali zikiwemo vyombo vya ndani
pamoja na mashine. “Pia itatuwezesha kwenda kujifunza na kukutana na
wazalishaji wenyewe bila kupitia kwa madalali wowote hivyo itatusaidia
kununua bidhaa kwa bei nafuu na kuja kuziuza nchini kwa bei nafuu pia,”
alisema Sipemba.